Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Pascal Lesoinne (wa pili
kushoto) Diwani wa Kata ya Wazo, John Moro (kushoto kwake) wakikata
utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Wazo Misikiti
na PK Tegeta itakayojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya uzinduzi
ilifanyika Wazo Hill nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wengine kutoka
kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa TPCC, Natasha D’Souza, Mkuu wa
Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Jayne Nyimbo na Mwenyekiti wa Mtaa wa
Wazo, Mtuzya Abdallah ,Mtuzya. Ujenzi huo utagharimu shs milioni 175.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Pascal Lesoinne
(katikati) akibadilishana mawazo na Diwani wa Kata ya Wazo, John Moro
muda mfupi kabla ya hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya
Wazo Misikiti na PK Tegeta itakayojengwa na kampuni hiyo. Hafla ya
uzinduzi ilifanyika Wazo Hill nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kulia
ni Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Ibrahim Mabewa. Ujenzi huo utagharimu
shs milioni 175.
Baadhi
ya wananchi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa
barabara ya Wazo Msikiti na Tegeta PK itakayojengwa na kampuni ya Twiga
Cement.
Credits: sufiani mafoto
Post a Comment