Habiba
Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa
hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za
haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mwenye
umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na wazazi wake kwa kipindi cha
miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa matunzo muhimu hali ambayo
imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo jijini mbeya katika
mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa karibu na mtoto huyo
pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani anapoishi mtoto huyo
kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika kwa jina la Joshua Joseph
umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya miaka miwili au mitatu ambaye
alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake wakiwa wameondoka
kuelekea kwenye shughuli zao .
Akizungumzia tukio hilo Kaimu barozi wa mtaa huo
wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali hiyo imenza kujitokeza kwa kipindi
cha miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi ya
utapiamlo.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2011 mwezi wa
tatu alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo ambapo
baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa lengo
la kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
Aidha baada ya kuhojiwa alikiri kosa
ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka kuhakikisha anamtunza
vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora pamoja na huduma nyingine.
.
Mara baada ya mtu huyo kupewa kalipio na
viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao kama viongozi wa shina
pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake aitwaye Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo
kwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo walikaidi agizo hilo.
Amesema mara baada ya watu hao kugoma
waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi wao na kuto watambua
tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao vya kikatili dhidi ya
mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa maaendeleo ya jamii kata
ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika katika eneo hilo wamesema kuwa
matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ndani ya jamii hasa kwa
vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao Ndugu Habiba Ibrahimu
amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa hivyo halipaswi
kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili
kuokoa maisha ya mtoto huyo
Amesema hali ya kiafya ya mtoto si ya kulizisha
kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali yanayotokana na kukosekana kwa
lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru majirani pamoja na viongozi
wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa karibu na mtoto huyo kwa kipindi
chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa ushirikiano toka kwa
wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika kituo cha afya
Inyala Kata ya Iyunga jijini hapa.
Awali inaelezwa kuwa baba na mama wa mtoto
huyo wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa kutokana na kutokuwepo
kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba huyo kuoa
mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama mama wa kambo.
Amesema kutoka na kuwepo kwa mgawanyiko huo
ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni mke wa pili walichukua
jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke wa kwanza ambapo kwa
asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa hali hiyo ya manyanyaso ya
mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo la kumtoa mtoto huyo
ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo hayo ya nyumbani ambapo
maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua kuchukua jukumu la
kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo Kata ya Iyunga kwa
lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbua mtoto huyo
Picha na Mbeya yetu
|
Post a Comment