Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Polisi walionaswa wakisafirisha bangi watajwa ..... Majina yao haya hapa







Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
**********

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, amewataja polisi wawili na gari la jeshi hilo ambalo walilitumia kusafirisha magunia 18 ya bangi kwenda Holili mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Aliwaja wkuwa ni dereva wa gari hilo Koplo Edward lenye namba za usajili PT 2025 aina ya Toyota Landcruiser linalotumiwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani
hapa, na mwenzake PC George namba za polisi G 2434.

Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakama ya kijeshi baada ya taratibu kukamilika.
Kamanda Sabas alisema jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu baadhi ya polisi wanaojihusisha na biashara hiyo tena kwa kutumia magari ya serikali.

Alisema baada ya taarifa hizo, walijipanga kwa kushirikiana na wenzao
wa mkoani Kilimanjaro na kuweka mtego uliofanikisha kuwanasa saa 5:00 usiku wakiwa katika Mji mdogo wa Himo.

Alisema gari walilokuwa wakiendesha lilikuwa limesheheni magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wakiyasafirisha kwenda Holili kwa lengo la kuuza kwa wafanyabiashara wa nchi jirani.
 
SOURCE::NIPASHE
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top