Imetangazwa
kwenye BBC NEWS WORLD zikithibitisha siku ya Rais wa Marekani, Barack
Obama kuja Tanzaniaitakuwa ni tarehe 1/06/2013White House inasema rais wa Marekani Barack Obama atakwenda Afrika mwishoni mwa mwezi wa sita ambapo atazuru nchi tatu.
Katika taarifa Jumatatu jioni, White House ilisema rais Obama na mke wake Michelle watakwenda Senegal, Afrika Kusini na Tanzania mwishoni mwa Juni na mapema mwezi Julai.
Utawala wa rais Obama unasema rais huyu wa Marekani atakutana na maafisa wa serikali, viongozi wa kibiashara, asasi za kiraia na makundi ya vijana.
Safari ya bw.Obama itaanza Juni 26 mpaka Julai 3 na inalenga kudhihirisha mahusiano ya karibu kati ya Marekani na nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.
Rais Obama ambaye baba yake alizaliwa Kenya, alizuru Afrika mara moja katika muhula wake wa kwanza, alipotembelelea Ghana mwaka 2009.
Mkewe Michelle Obama pia amesafiri kwenda Afrika Kusini na Bostwana.

on Tuesday, May 21, 2013
Post a Comment