Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania,
Barbara Kambogi akiwakaribisha wageni wanahabari katika hafla mchapalo ya
kusheherekea Africa Day na Dstv ambapo amesema DStv inatoa nafasi kwa wateja
wake kuwa na fursa ya kuchagua vifurushi mbalimbali kulingana na uwezo wa mteja
ambacho cha uwezo wa chini kabisa ni Access chenye zaidi ya channeli 40 gharama
yake ni nafuu sana ambapo mteja atalipia shilingi 16,500 kwa mwezi. (Picha na Zainul Mzige wa
dewjiblog).

Meneja wa Fedha wa kampuni ya Multichoice
Tanzania, Bw. Francis Senguji akizungumzia malengo ya DStv Tanzania ambapo
amesema wao kama waendeshaji wa biashara nyingine barani Afrika wanaojali na
kuthamini maendeleo ya jamii wameona ni wajibu kusaidia jamii ili kuweza
kuendeleza maendeleo ya kijamii nchini Tanzania.
Kwa kuendeleza hilo Multichoice ina mfumo
wa kutoa elimu mashuleni ( Multichoice Resource Centre) hivyo watamumia jukwaa
la Teknolojia kama darasa kwa njia mbalimbali kuwapa jamii nafasi ya kuendeleza
vipaji na ujuzi.
Mfumo huo kutoa rasilimali kwenye shule
kama vile ving'amuzi vya Satellite, VCRs/DVD na kifurushi cha elimu cha Dstv.
Mpaka sasa Multichoice imeanzisha vituo vya rasilimali jamii katika shule 82
nchi nzima kwenye mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Mbeya,
Pwani na Tanga.

Meneja Uendeshaji wa Multichoice
Tanzania, Ronald Shelukindo (katikati) akifafanua jambo wakati wa hafla mchapalo
katika kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv. Kulia ni Meneja Masoko wa
Kampuni hiyo Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Barbara
Kambogi.

Waalikwa katika hafla mchapalo ya
kusheherekea usiku wa Africa Day na DStv katika Hoteli ya New Africa ya jijini
Dar usiku wa kuamkia leo.

Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa
Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Blogger John Bukuku wa Fullshangwe Blog,
Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo Ronald Shelukindo, Mdau wa DStv na Meneja wa
Fedha katika kampuni hiyo Bw. Francis Senguji wakipozi kwa
picha.

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania,
Barbara Kambogi (kulia) akifurahi jambo Wanahabari Sidi Mgumia (katikati) na
Mama Mhina.

Ronald Shelukindo na Mdau LEMUTUZ wa Blog
ya jamii.

Kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa
Multichoice Tanzania Furaha Samalu, Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo Ronald
Shelukindo, Meneja wa Fedha katika kampuni hiyo Bw. Francis Senguji na mdau wa
DStv wakipozi mbele ya camera yetu wakati wa hafla ya kusheherekea African Day
na DStv iliyowakutanisha waandishi wahabari kutoka vyombo mbalimbali
nchini.

Bloggers wakishow love...Kutoka kushoto
ni Mkurugenzi wa Fullshangwe Blog John Bukuku, William Malecela wa Blog ya
wananchi a.k.a LEMUTUZ na Operations Manager wa Mo Blog Zainul Mzige a.k.a
Bigzee katika hafla mchapalo ya kusheherekea African Day na DStv katika Hoteli
ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Wanahabari wakiwa bize kujaza Quiz
iliyotolewa na kampuni ya Multichoice Tanzania ambapo mshindi kwanza amezawadiwa
Full Set ya King'amuzi cha Dstv na 'Subscription' ya mwezi mmoja na washindi
kumi wamezawadiwa kofia na T-shirts za Supersport moja ya chaneli zinazopatikana
katika king'amuzi cha Dstv.

Wanahabari wakiendelea kuumiza kichwa
huku wengine waki-google majibu ya Quiz hiyo kupitia simu zao za
kiganjani.

Mtangazaji wa Radio Dennis Buslwa a.k.a
Ssebo (kulia) akiwa busy kutafuta majibu ambapo tunahisi alikwa anawasiliana na
watu wa Mo Blog wampe majibu kamili. Wengine ni Kamera Man wa Channel Ten na
Mtangazaji wa Radio Salma Msangi pamoja na mdau wa Star Tv.

Barbara Kambogi akiteta jambo na Angela
Msangi wa TBC.

Dada Revina Bandihai wa kampuni ya
Multichoice Tanzania na HR Manager wa kampuni hiyo.

Ronald Shelukindo na Dada Furaha Samalu
wakifungua mziki wa Kiafrika huku Bw. Francis Senguji akiserebuka na
mdau.

Mkurugenzi wa Fullshangwe Blog John
Bukuku akiserebuka na Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi
wakati wa hafla hiyo.

Salma Msangi akionekana Kiafrika zaidi
akiyarudi na Khadija Kalili wa Jambo leo.

Kwaito ilichezeka kisawa sawa....Chezea
Multichoice wewe.....Ilinogaje.!

Kutoka kushoto ni Blogger Cathbert Angelo
wa kajunason Blog, Mpiganaji Fadhili Akida na Blogger Othman Michuzi wa mtaa kwa
mtaa Blog wakipoowz mbele ya kamera yetu.

Bloggers katika picha ya
pamoja.

Dada Revina Bandihai wa Multichoice
Tanzania na Bw. Francis Senguji wakisataka Rhumba wakati wa hafla
hiyo.

Meneja wa Fedha wa Multichoice Tanzanua
Bw. Francis Senguji akimpongeza Ssebo baada ya kuibuka mshindi katika Quiz
iliyoendesha na Kampuni hiyo ambapo alinyakua Full Set ya King'amuzi cha Dstv na
'Subscription' ya mwezi mmoja.

Pichani juu na chini Meneja Uhusiano wa
Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akigawa Kofia na T-shirts kwa washindi wa
Quiz ilyoendeshwa na kampuni hiyo wakati wa kusheherekea Africa Day na
Dstv.


Dada Revina Bandihai (kushoto) wa
Multichoice Tanzania akishow love na washindi wa Quiz iliyoendeshwa na kampuni
hiyo.

Wanahabari wakishow love...Thank you DStv
for the Cocktail Party to celebrate Africa Day with
DStv.


Post a Comment