Mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama mkoani Singida, Edward Ole Lenga.(Picha na Nathaniel Limu).
***********
Na Nathaniel Limu.
Mwalimu
wa shule ya msingi kata ya Msingi tarafa ya Kinampanda wilayani Mkalama
Wolter Ponela (32) anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya
wilaya ya Iramba, kujibu tuhuma ya kumjaza mimba mwanafunzi wa kidato
cha pili mwenye umri wa miaka 17.
Mwanafunzi huyo anasoma katika shule ya sekondari Jerumani iliyopo kata ya Msingi.
Mkuu
wa wilaya ya Mkalama Edward Ole Lenga amesema ofisi yake imesikitishwa
na kitendo cha mwalimu huyo kwa madai kuwa kinachangia kuharibu maisha
ya msichana husika.
Amesema
vitendo hivyo ni lazima vipingwe vita na wadau wote ili kuhakikisha
wanafunzi wa kike wanasoma hadi upeo wao bila vikwanzo.
Katika
hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya amekemea vikali tabia iliyoota
mizizi ya kumaliza kienyeji matatizo ya wanafunzi kubebeshwa mimba.
Lenga
amesema ni lazima sheria zilizowekwa zitumike katika kukomesa tabia za
kuwajaza mimba wanafunzi ambazo huwa hazitarajiwi au mimba za utotoni.
Aidha,
ameagiza watendaji kila moja katika maeneo yake aorodheshe majina ya
wanafunzi waliojazwa mimba na watu waliochangia uharibifu huo wa mimba
za utotoni.
Lenga
amewataka walimu kutenga muda kuwaelimisha wanafunzi wa kike madhara
yatokanayo na mimba za utotoni kama njia moja wapo itakayosaidia
wanafunzi kuchukia vitendo vya mahusiano ya kimapenzi wakati wakiwa
wangali shuleni.
Post a Comment