RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
KUZINDUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA – IRINGA YENYE UREFU WA
KM 260 (SEHEMU ZA DODOMA – FUFU ESCARPMENT, FUFU ESCARPMENT – MIGORI NA
MIGORI – IRINGA) KWA KIWANGO CHA LAMI TAREHE 22 MEI, 2013
Wizara
ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, tarehe 22 Mei, 2013
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya
ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:-
1) Tarehe 22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment (km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.
2)
Tarehe 22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu
Escarpment – Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji
cha Migori Wilayani Iringa Vijijini.
Barabara
ya Iringa – Dodoma ni sehemu ya barabara muhimu ijulikanayo kama “Great
North Road” inayoanzia Capetown Afrika ya Kusini hadi Cairo, Misri
kupitia Tanzania. Nchini Tanzania inaunganisha Miji ya Tunduma (mpakani
na Zambia), Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha na Namanga (mpakani na Kenya).
Mradi
huu ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha
miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara na unalenga kupanua fursa za
kiuchumi na kibiashara kwa wananchi, na kati ya Tanzania na nchi jirani
za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC). Kwa njia hii, barabara itakuza uchumi wa wananchi na
Taifa kwa ujumla.
Taarifa hii imetolewa na
Balozi Herbert E. Mrango
KATIBU MKUU
WIZARA YA UJENZI
Post a Comment