Habari
zilizotufikia toka IFM- Dar es salaam ni kwamba mwanafunzi mmoja
ambaye bado hatujafanikiwa kulipata jina lake amefariki dunia
kwa kulishwa sumu katika chakula alicholetewa na mpenzi wake
ambaye ni mke wa mtu......
Taarifa
zaidi zinadai kwamba Mwanafunzi huyo alikuwa na uhusiano wa karibu
sana na mke wa mtu ambaye mbali na starehe za kimapenzi alikuwa
pia anampekea chakula cha jioni
Baada
ya mchezo huo kudumu kwa muda, mume wa mwanamke aliusoma
mchezo mzima na kuandaa tego la kuwaangamiza wote....
Habari
zinadai kwamba Siku ya jumatano jioni mwanaume huyo aliwahi kurudi
nyumbani na kufanikiwa kukinasa chakula kilichokuwa
kimeandaliwa tayari kwa kupelekwa kwa huyo mwanafunzi ambaye
alikuwa anatembea na mke wake.....
Baada
ya kukinasa, alijifanya kuzuga na kupotezea...Mkewe alipotoka
alikichukua na kukitia sumu chakula hicho na kisha kukiweka
kama kilivyokuwa kimeandaliwa....
Lengo lake lilikuwa ni kuwamaliza wote maana alijua ni lazima akifika watakaa na kula pamoja.....
Mwanamke
alipopeleka chakula hakukaa kula na badala yake alimwambia yule
mwanafunzi kuwa mume wake amewahi kurudi siku hiyo hivyo hatoweza
kukaa wale pamoja....Mwanafunzi huyo akakipokea na kukila na
ndipo mauti yakamkuta
Habari
toka chuoni hapo zinadai kwamba mwanafunzi huyo alikuwa
ameshadisco lakini alikuwa amepewa nafasi nyingine ya kurudia
mwaka wa pili , hivyo aliendelea kukaa mtaani kama mwanafunzi....
Mwili wa marehemu bado uko Muhimbili kwa uchunguzi zaidi baada ya polisi kuuzuia kuzikwa....
Hizi
ni habari mbaya sana kwa wanafunzi wa chuo hicho maana ni
jumatatu tu mwanafunzi mwingine alifariki katika hali ya
kutatanisha baada ya kifo cha mpenzi wake miezi michache
iliyopita....
Habari
za ndani zaidi zinadai kuwa toka mwaka huu uanze mpaka sasa chuo
cha IFM kimepoteza wanafunzi 12 huku wawili wakiripotiwa kuwa na
hali mbaya zaidi katika hospitali ya Muhimbili....
Mtandao huu unaendelea kuifuatilia habari hii kwa kina zaidi
Post a Comment