Bodi
ya Mapato ya Zanzibar (ZRB), imetoa amri ya kuzuia kutua na kuruka kwa
ndege za kampuni ya Precision Air Service Co. Ltd, katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, kutokana na kutolipa zaidi ya Sh bilioni
37.2 zinazotokana na malimbikizo ya malipo ya ada ya huduma ya uwanja wa ndege.
Amri
hiyo iliyopatikana jana, imetolewa na Kamishna wa Bodi ya Mapato ya
Zanzibar, Abdi Faki, Aprili 25 mwaka huu kutokana na malimbikizo hayo.
“Chini
ya kifungu cha 43(1) cha taratibu na udhibiti wa kodi cha mwaka 2009,
mimi Abdi Faki, Kamishna wa Bodi ya Mapato ninatoa amri ya kuzuia kuruka
na kutua kwa ndege za kampuni ya Precision Air Service Co. Ltd kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kuanzia saa saba usiku wa
Aprili 25 mpaka hapo watakapolipa fedha hizo.” Mbali na amri hiyo, pia ZRB inakusudia kufunga ofisi zote za kampuni hiyo zilizopo Zanzibar.
Faki
alisema kuwa Precision Air Service Co. Ltd, imeshindwa na kupuuzia
kulipa deni la zaidi ya Sh milioni 144.8 na zaidi ya dola za Marekani
347,066 (zaidi ya Sh milioni 520.6), kama malipo ya makato ya huduma za
viwanja na usalama kwa miezi mitatu tangu Januari hadi Machi mwaka huu.
Alisema
pia kampuni hiyo imeshindwa kulipa zaidi ya Sh milioni 70.5 na zaidi ya
dola za Marekani milioni 1.6 (zaidi ya Sh bilioni 2.5), kama fedha za
adhabu kutokana na ucheleweshwaji wa malipo kuanzia Februari hadi Agosti
mwaka 2012.
“ZRB
imekuwa ikiwakumbusha Precision Air Service Co. Ltd mara kwa mara ili
kulipa deni hilo, lakini wameshindwa na kupuuzia suala hilo. Sheria
inatutaka kufuata utaratibu wa kukusanya na kulinda mapato ya Serikali,”
alieleza.
Faki
alisema Precision Air iliteuliwa na Waziri wa Fedha kukusanya malipo ya
huduma na usalama kwenye uwanja za ndege wa kimataifa wa Zanzibar,
chini ya kifungu namba 2 ya mwaka 1999 na sheria namba 34 ya mwaka 2007.
Alisema
tabia ya makusudi ya kupuuza na kuacha kufanya mawasiliano ya kiofisi
na kutolipa malipo ya ada, inayofanywa na kampuni hiyo, ni uvunjwaji wa
Sheria ya Ukusanyaji wa Mapato ya mwaka 2009, gharama za huduma za ndege
ya mwaka 1999 na gharama za huduma ya uwanja na wakala wa usafirishaji
ya mwaka 2007.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha Precision Air, Patrick Ndekana, alipoulizwa alisema sio kweli kuwa ndege zao zimefungiwa. “Sio
kweli kuwa ndege zetu zimezuiliwa kutua na kuruka Zanzibar. Mpaka muda
huu ninaozungumza nawe (saa 11 jioni) kuna ndege yetu inajiandaa kuruka
kutoka Zanzibar,” alisema Ndekana.
Kuhusu
kudaiwa zaidi ya bilioni 37.2, Ndekana alisema hana taarifa na kuongeza
kuwa hilo ni suala la watu wa fedha na kuahidi kulitolea ufafanuzi
zaidi.
source zero99
Post a Comment