Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWANDISHI CHARLES MULINDA AJITOA JUKWAA LA WAHARIRI .... SABABU ZA KUFANYA HIVYO HIZI HAPA

 


8 c1dd8
Charles Mullinda

Mhariri Mtanzania Jumatano
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la WahaririYAH: KUJITOA KWENYE JUKWAANapenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.Nimeamua kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini hayapaswi kufumbiwa macho.
Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.Aidha, siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.
Kikao cha kwanza na TEF na kilichofanyika leo kimedhihirisha pasipo mashaka kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda maalumu ya kumshughulikia Mullinda kwa kuwa tu nilionyesha mawasiliano ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo dhidi ya Ludovick kama ambavyo gazeti la Tanzania Daima lilivyoonyesha mawasiliano ya Dennis Msaki na Ludovick..
Ripoti ya timu iliyoundwa kuchunguza ukweli wa habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania Jumatano ina upungufu mkubwa wa kimantiki ambao hata kwenye kikao niliuonyesha lakini haukusikilizwa.Ushahidi wa Ngurumo kumtuma pesa Ludovick upo wazi, lakini hakuna mtu anayeliangalia hilo kwa sababu tu timu ile iliundwa kumshughulikia Mullinda kwa sababu aliandika vigogo wa TEF ambao wako karibu na viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.
Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana utazingatiwa.Charles Mullinda.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top