MBUNGE wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani (CCM), amesema kuwa yuko tayari kujiuzulu ubunge endapo madai yanayotolewa na wapinzani wake wa kisiasa kuwa amekuwa akifadhili genge la wahuni kuendeleza mgogoro wa Wakulima na Wafugaji.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Ngonyani (Profsa Maji Marefu), alisema wema wake katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo kwenye kijiji cha Magamba kwa Lukonge ndio unaomponza.
Alisema kunakikundi cha baadhi ya wafugaji ambao ndio chanzo cha mgogoro huo tangu miaka 15 iliyopita kuwa wamejipanga kwenda kumshtaki kwa rais Jakaya Kikwete mbunge huyo kutokana na kupendelea upande mmoja.
“Mimi nilikuwa mstari wa mbele katika kusimamia mgogoro huo ili wananchi hao waweze kuishi kwa amani na mimi nimechaguliwa na wananchi wote wafugaji na wakulima sasa itakuwa ajabu kuukandamiza upande mmoja hii si tabia yangu”alisema.
Ngonyani alisema kutokana na mgogoro huo ambao umekuwa ukichochewa na baadhi ya wanansiasa aliowashinda kwenye uchaguzi mwaka 2010, yuko tayari kujiuzulu ubunge endapo madai hayo yanayopelekwa kwa Rais yakithibitika yana ukweli.
“Hivi karibuni wakati nikiwa bungeni nilipata taarifa kuwa kuna mfugaji aliingiza ng’ombe wake kwenye shamba la mkulima lenye heka sita ambako ng’ombe hao waliharibu mazo yote kitendo kilichozua vurugu”alisema.
Kutokana na hali hiyo, ilimbidi kurudi jimboni kwake kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi ambapo alikutana na Mkuu wa Wilaya pamoja na pande zinazohusika kutafuta ufumbuzi wa kumaliza mtafaruku huo.
Katika hali ya kushangaza kuna taarifa zilizoandikwa na gazeti moja (si hili), kuwa yeye alkuwa akikifadhili genge lililojulikana kama ‘Mungiki’ kuwafanyia vurugu wafugaji kitendo mbacho si kweli.Aliongeza kuwa haitatokea kuungana na watu wanaoendesha vurugu katika jimbo hilo vilevile aliwataka baadhi ya wanasiasa kuacha kudumisha migogoro kwa ajili ya kujipatia umaarufu.
Credits: Fullshangwe blog
Post a Comment