Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ikulu jijini Dar es Salaam amemwapisha
Jaji Aloycius Mujuluzi kuwa Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria
pamoja na mabalozi wanne watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.Mabalozi
walioapishwa leo ni pamoja na Balozi mpya katika umoja wa Falme za
kiarabu(UAE) Mbarouk Nassor Mbarouk,Balozi mpya wa Tanzania nchini
Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya
Commoro Chabaka Kilumanga na Mwakilishi wa kudumu Tanzania Umoja wa
mataifa Geneva Balozi Modest Jonathan Mero.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na
Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na
mabalozi wapya waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama
mbele kushoto no Balozi Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa
Tanzania nchini Marekani.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya
wa Tanzania Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi mpya wa Tanzania katika
visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga,Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania
Umoja wa Mataifa Geneva Balozi Modest jonathan Mero na Balozi mpya wa
Tanzania katika falme za Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor Mbarouk.Kabla ya
uteuzi Balozi Liberata Mulamula alikuwa msaidi wa Rais Masuala ya
kidiplomasia na aliwahi kuwa katibu mkuu wa nchi za Maziwa Makuu.(picha
na Freddy Maro)
Balozi Kilumanga-Commoro Akiapa
Balozi Masilingi-Uholanzi akiapa
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (UAE) akiapa
Balozi Mero-Geneva akiapa
Jaji Aloycius Mujuluzi akiapa
Post a Comment