TAMASHA la
Mastaa chipukizi zaidi ya 320 la mwezi Mei litafanyika Jumapili 26,
2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10
jioni.
Mwenyekiti
wa Shiwata, Caasim Taalib alisema maandalizi ya tamasha hilo
yamekamilika na vikundi vya sanaa vya Kaole, Splendid, Super Shine
Taarab, Five Star Modern Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo
Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.
Taalib
alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas,
Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao
katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .
Vikundi
vingine vitakaonesha vipaji vyao ni Kepteni Shaibu, Tanzania Disabled,
Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts
Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata
Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na
Begeja Wushu,
Wakati
huo huo SHIWATA inawapongeza wote walioshiriki tamasha la Aprili 27
ambako zaidi ya wasanii 300 walishiriki kuonesha vipaji.
Pia
Taalib amelipongeza Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa ushirikiano
wao mzuri na kuwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki,
taarab,vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki
katika matamasha haya ili kujenga ushirikiano wa pamoja.
Post a Comment