Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) akipokewa na Mkuu wa Kitengo
cha Huduma za Fedha zinazofuata Kanuni za Kiislamu ‘NBC Islamic
Banking’ cha Benki ya Taifa ya Biashara, Yassir Masoud alipokwenda
kufungua semina ya siku moja kwa wanawake wajasiriamali waislamu
iliyoandaliwa na NBC mjini Tanga leo. Katikati ni Meneja Tawi la NBC
Tanga Deusdedit Mashalla.
Baadhi
wa washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Benki ya NBC
Kitengo cha Islamic Banking wakiwa katika semina hiyo jijini Tanga leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua semina ya siku moja kwa
wanawake wajasiriamali waislamu iliyoandaliwa na Benki ya NBC Kitengo
cha Islamic Banking mjini Tanga LEO. Kulia ni Mkuu wa kitengo hicho,
Yassir Masoud na kushoto ni Meneja Operesheni wa NBC Tawi la Tanga
Kibibi Said Kibao.
*****
Na Mwandishi Wetu
Benki
ya Taifa ya Biashara (NBC) kupitia kitengo chake cha Huduma za Kibenki
zinazofuata kanuni za kifedha za Kiislamu inatarajia kuanzisha huduma ya
mikopo kwa wafanyakazi ‘Islamic Group Finance’ kabla ya Septemba mwaka
huu.
Akizungumza
wakati wa semina ya siku moja ya wanawake wajasiriamali wa Kiislamu
jijini Tanga jana, Mkuu wa Islamic Banking wa NBC, Yassir Masoud alisema
lengo la kuanzishwa kwa huduma hiyo ni kutoa fursa za mikopo kwa wateja
wao wanaohudumiwa kwa kufuata kanuni za dini hiyo.
Masoud
aliwaambia wanawake waliohudhuria semina hiyo kwamba ili waweze
kujikwamua kiuchumi, wanahitaji kujifunza mbinu za biashara, akisisitiza
kwamba hata mafundisho ya Kiisllamu yanatoa maelekezo kuhusu utafutaji
wa riziki.
”Uislam
umehimiza mambo ya uwekezaji, Uislamu unahimiza masuala ya mali
maandiko yakisema kwamba kutafuta riziki ni sawa na kutafuta fadhila za
Mwenyezi Mungu,” alisema.
Akifungua
semina hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku Galawa aliwahimiza
wanawake mkoani humo kujizatiti kwenye ujasiriamali ili kusaidia juhudi
za serikali katika kuinua maendeleo yasiyoridhisha ya mkoa huo.
Alisema
kuwa kwa kupitia semina hiyo, NBC imefungua njia mpya yenye matumaini
kwa wanawake wa Tanga, njia ambayo mashirika mengine yanapaswa kuifuata.
“NBC
ni moja kati ya benki kongwe yenye mtanda mpana kuliko zote nchini na
imekuwa mstari wa mbele ikishirikiana na watu mbalimbali katika
kuboresha maisha ya Watanzania,” alisema.
Katika
siku za hivi karibuni, NBC imekuwa ikiwekeza zaidi katika kuelimisha
jamii, hususan wajasiriamali kupitia semina na warsha mbalimbali huku
ikishirikiana na makampuni mengine.
Mwishoni
mwa mwaka jana, benki hiyo iliandaa mkutano wa wajasiriamali wadogo
wadogo wa jijini Dar es Salaam kwa ushirikiano na shirika lisio la
kiserikali linalojishughulisha na vijana, YESi.
NBC
pia ni wadhamini wa Top 100 Midsize Companies Survey ambayo inaendeshwa
kwa ushirikiano na KPMG kuyasaka na kuyazawadia makampuni ya kati
yanayokuwa kwa kasi.
“Sekta
ya Biashara ndogo ndogo na za kati ni muhimu katika kukuza uchumi
nchini, na ni sekta inayoweza kutoa nafasi za ajira kwa wananchi wengi.
NBC wametambua hilo,” alisema.
Aliishukuru
benki hiyo na kuishauri iendelee kutoa mafunzo kwa wahusika wa sekta
hiyo na kuwawezesha wajasiriamali kukuza biashara zao na hatimaye kuinua
uchumi wa nchi.
Post a Comment