SIKU chache kufuatia askari wa tatu wa Jeshi la Polisi wa kituo cha
Dumila wilayani Kilosa na Dakawa wilayani Mvomero, mkoani Morogoro
kutuhumiwa kumbambikizia kesi mfanyabiashara Samson Mwita maarufu kama
Mura, mkazi wa Dumila kuwa alikutwa na fuvu la kichwa cha binadamu,
hatimaye askari hao wamefukuzwa kazi rasmi na kufun
guliwa mashtaka mahakamani.
Jeshi hilo limesema askari hao wamefukuzwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fausitine Shilogile (pichani), alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya uchuguzi kukamilika na askari hao kubainika kufanya upekuzi kwa mfanyabiashara huyo bila kuwa na kibali kutoka kwa wakuu wao wa kazi.

Alisema askari hao walifikishwa katika mahakama ya kijeshi na kubainika kufanya kitendo hicho na kuvuliwa uaskari na kwamba tayari wamefikishwa katika mahakama ya kiraia na kesi yao kwa mara ya kwanza inatarajiwa kusomwa Juni 3 katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro.
Aliwataja askari hao kuwa ni mwenye namba D 4807 D/SSGT Sadick wa kituo kidogo cha Polisi Dakawa, E 4344 SGT Mohamed na E 3821 CPL Nuran wote wa kituo kidogo cha polisi Dumila.
Alisema kuwa askari hao walifanya tukio hilo Mei 7, mwaka huu majira ya asubuhi katika kijiji cha Mgudeni Dumila wilayani Kilosa kwa kujaribu kumbambikizia kesi ya kukutwa na fuvu la kichwa kinachodaiwa kuwa cha binadamu mfanyabiashara huyo kwa lengo la kujipatia fedha.
Alisema uchunguzi umebaini kuwa askari hao walifanya kitendo hicho kwa kushirikiana na raia Rashidi Ally (47)mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam.
Credits: Jumamtandablog
Post a Comment