KATIKA
hali isiyo ya kawaida nchini, baadhi ya wabunge wameyatelekeza majimbo
yao kwa kutorudi kusikiliza kero za wananchi na kutimiza ahadi zao.
Imefikia
baadhi ya wanasiasa wanadhani majimboni ni sehemu ya kuchota kura na
kuwaacha wananchi waendelea kubaki kama walivyo kana kwamba wapo
kisiwani kusiko na msaada, huku hawajui ni lini wataokolewa labda pale
tu watakapofanya maamuzi magumu ya kuitosa.
Wananchi
katika Majimbo mbalimbali nchini wamemekuwa wakilia na tabia ya wabunge
wao waliowachagua ili wawawakilishe bungeni, kwa bahati mbaya baadhi
yao wamekuwa wasaliti kwa wapiga kura wao, kutokana kuonekana mara
chache kwenye majimbo yao.
Hali
hiyo imewapelekea wakiwa wabunge hao wakiwa bungeni, hulipuka kusema
mambo ambayo hawakuagizwa na wapiga kura, kitendo ambapo muda wao
huishia kuwashukuru wake zao, kutukana matusi, sanasana kulala usingizi,
bila kusemea kero za majimboni mwao.
Kutokana
na wabunge kuasi majimboni kuongee na wapiga kura nini wakazungumze
bungeni dhidi ya kero zinazowasibu, utashangaa wanabakia kusikiliza
wapinzani wamepinga kitu gani ili waanze kuwashambulia, badala ya
kuwatetea wapiga kura wao.
Uchunguzi
ambao umefanywa na kubaini mapungufu kadhaa ya wawakiliishi hawa,
wabunge karibu wote imebainika wanakwenda mara chache sana majimboni
mwao, na wanaweza kwenda na wasifanye mikutano yoyote, jambo
linalowaudhi wananchi.
Kuthibitisha
malalamiko ya wapiga kura na wananchi wa baadhi ya majimbo, ukichunguza
kwenye mahudhurio yao kwenye vikao vya DCC na RCC, wabunge hao ni nadra
kuhudhuria kwenye vikao hivyo.
Mara
kadhaa ukisoma kwenye mihutasari utaona labda ni mbunge mmoja tu
alikuwepo, lakini wengine wote utakuta imeripotiwa ni udhuru tuuu, jambo
ambalo linawakasirisha sana wapiga kura na wapenzi wa vyama husika.
Mwananchi
mmoja wa Mvomero ambaye ni Kiongozi wa Chama kinachotawala (CCM)
aliyeomba asitajwe jina lake kwa kuhofia kukemewa alichodai ni
kukolimbwa kwa kudai haki alisema, ”Tumechoshwa na wabunge wanaojifanya
wazaliwa wa wilaya na mikoa ya maeneo yetu, na baadaye wanahamishia makazi na shughuli zao Dar es Salaam.
“Kimsingi
tunatafakari kwa umakini Udanganyifu huu na Usanii tunaofanyiwa na
baadhi ya wabunge wetu, kuchota kura na kamwe tutaendelea kubaki kama
tulivyo kama watu walio kwenye kisiwa na hatujui lini tutaokolewa labda
pale watakapofanya maamuzi magumu ya kuitosa CCM mwaka 2015”.
Wakati
wapiga kura wakiwalalamikia wabunge wasiochukua maoni yao na kuwatetea
bungeni, Rais Dk. Jakaya Kikwete kwenye kikao chake na wabunge wa CCM
Dodoma hivi karibuni, amekea tabia ya wabunge watoro wasiotembelea
majimbo yao.
Katika
kikao hicho kilichofanyika mjini Dodoma, Imefahamika Rais amekaririwa
akisema baadhi ya wabunge wameyatelekeza majimbo yao kwa kutorudi
kusikiliza kero za wananchi na kutimiza ahadi zao, kitendo ambacho ni
hatari kwa wao kurudi kwenye majimbo yao na CCM.
Hivi
karibuni bila ya kuuma uma maneno kwa Mkutano wa hadhara, Naibu Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe
amewachongea Wabunge wa Mkoa wa Tabora (CCM) kwa wananchi, akidai ni
wasaliti kwa wapiga kura wao, ambapo baadhi ya wananchi walimuunga
mkono.
Ni
rai yangu Wabunge wa namna iliyoelezwa, wajikague wajitathimini, ili
wasiwe watoro majimboni na kuwa Viwete, Bubu, Vipofu na wagumu wa
kuwatetea wapiga kura wao, ingawa ni rahisi kudai posho zao,
wanahatarisha uwakilishi wao 2015.
0715-933308
Post a Comment