Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali yatenga fedha kununua mashine mpya ya CT- Scan Muhimbili.



Na Immaculate Makilika- Dodoma
imagesSERIKALI imeeleza kwamba Wizara ya Afya katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 imetenga fedha kwa ajili ya kununua mashine mpya ya CT- Scan ya kisasa zaidi na yenye uwezo mkubwa(250 slices) ili kuimarisha huduma katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH).
Aidha Serikali imefafanua katika mwaka 2012/2013 mashine ya CT- Scan ya MNH, ilikuwa imeharibika kwa takriban miezi 11,hali iliyosababisha kuwepo kwa mrundikano wa wagonjwa waliohitaji huduma ya kipimo cha CT-Scan.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alipokuwa akijibu swali la Mussa Zungu(CCM) alilouliza kwa niaba ya Al- Shaymaa Kwegyir(Viti Maalum –CCM) kwamba je,ni kwanini imechukua muda mrefu kushughulikia tatizo linalowaumiza Watanzania ambao ni wanyonge na wanaolazimika kutoa gharama kubwa kwa ajili ya kipimo hicho.
Naibu Waziri wa huyo alisema ni kweli kwamba kutokana na ubovu wa mashine hiyo,baadhi ya wagonjwa walilazimika kutafuta huduma ya kipimo nje ya MN H ,ambapo gharama za kipimo ni kati ya sh.200,000/= hadi 300,000/= .Serikali imesikitishwa na adha waliyopata wananchi waliohitaji huduma hii na kushindwa kuipata.
Hata hivyo Dk. Rashid alisema matengenezo ya CT-Scan yalichukua muda mrefu kutokana na kwamba kampuni ya Philips Medical Services (PMS), ambayo ndio yenye mkataba wa matengenezo ya mashine za X-ray ikiwemo mashine ya CT- Scan,kulazimika kuagiza vipuri nje ya nchi kwa ajili ya matengenezo ya mashine hiyo.
Aidha alisema mashine ilikuwa modeli ya zamani (6 slices), upatikanaji wa vipuri ulikuwa mgumu .Taratibu za uagizaji na ununuzi wa vipuri zilifanyika na matengenezo yalikamilika mwishoni mwa Desemba ,2012.
Kwa sasa hivi mashine ya CT- Scan ya MNH, inafanya kazi vizuri ,na wagonjwa wanapatiwa huduma.Tatizo la mrundikano wa wagonjwa wa huduma hiyo halipo tena.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top