VIJANA wanne wa jamii ya kifugaji almaarufu (Morani) wilayani Ngorongoro wamejeruhiwa vibaya na simba huku mmoja wao akiwa mahututi kwenye hospitali ya Selian, Arusha baada ya mapambano ya kuokoa mifugo yao isiliwe na simba.
Vijana hao ni Jacob SADIRA alijeruhiwa vibaya, Lemberwa Ole-Napurda,Toto olenapurda na Orpenear Ole Nangokole na kwamba walikuwa wakijaribu kuwaokoa mifugo ambayo ilivamiwa na simba wanne.
Tukio hilo limetokea usiku wa mei 17 mwaka huu kwenye kijiji cha Kitumbaine wilayani ngorongoro baada ya simba hao kuvamia boma la kimaasai na kuanza kuwashambulia Ng’ombe wa familia ya vijana hao.
Kwa mujibu wa shuhuda wa habari hii katika mapambano hayo kijana mmoja aitwaye Jacob Sadira alijeruhiwa vibaya na simba hao katika mkono wake wa kulia na hadi jana majeruhi huyo alikuwa amelazwa katika hospital ya Selian inayomilikiwa na Kanisa la kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya kaskazini.
Baadhi ya majeruhi hao waliojeruhiwa kwenye kadhia hiyo ni Lemberwa Ole-Napurda,Toto olenapurda na Orpenear Ole Nangokole ambao walikimbizwa katika kituo cha Afya kitumbeine kwa matibabu zaidi.
Akizungumzia kadhia hiyo mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la ujamaa Trust Jamboi Baramaegu alisema kuwa tukio hilo ni mfululizo wa matukio ya uvamizi wa wanyama katika makazi ya watu au maboma ya wamaasai.
Baramaegu alisema kuwa hata hivyo hakuna hatua ziazochukuliwa kuwalipa fadia wahanga hao wa matukio kama haya huku watu wakiendelea kuathirika na uvamizi wa wanyama. Chanzo: Mahamoud Ahmad, Ngorongoro
Post a Comment