Vyombo
vya Habari nchini vimeaswa kutumia uhuru wake vizuri bila kusababisha
madhara ndani ya nchi kama ilivyotokea katika baadhi ya nchi za Afrika.
Akichangia
hotuba ya wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Jaddy Simayi
Jaddy mbunge wa Mkwajuni alisema baadhi ya vyombo vya habari vilivyopo
hapa nchini vinaweza kuchangia machafuko ndani ya nchi kwani mwelekeo
wa mambo yanayoandikwa yana dalili ya uchochezi.
Alisisitiza
kuwa hata kama wananchi wanavihitaji vyombo vya habari lakini
vikiachiwa vifanye vinavyotaka vitaipeleka nchi pabaya. “Ni kweli
tunavihitaji sana vyombo hivyo ila kwa sasa inabidi viangaliwe kwa
umakini sana” Alisema mchangiaji.
Aliiomba
Serikali iwasilishe sheria ya vyombo vya habari kama ilivyo ahidi ili
kuweza kudhibiti baadhi ya mambo yasiyo sahihi yanayoonekana kwa sasa
kwenye vyombo vya habari.
Akielezea
uwezo wa vyombo vya habari alisema vyombo hivyo vina nguvu kubwa katika
kujenga nchi na kuleta maendeleo ya nchi yeyote ile duniani.
Naye
Mbunge wa Bunda Mh. Stephen Wasira akichangia hoja hiyo alisema uhuru
lazima uwe na mipaka . Kama hakuna nidhamu ya vyombo vya habari uwepo wa
demokrasia inapotea.
Alisema
Tanzania ni kati ya nchi inayojali uhuru wa vyombo vya habari kwani
mpaka sasa ni nchi pekee Afrika Mashariki iliyo na vyombo vingi vya
habari. Takwimu zinaonesha mpaka sasa kuna jumla ya magazeti na majarida
781, magazeti yanayotoka kila siku 13 na magazeti na majarida
yanayotoka kwa wiki 62 na kuongeza kuwa hiyo ni moja ya mafanikio
makubwa ya kutekeleza uhuru wa Vyombo vya Habari nchini.
Hata
hivyo aliwaomba waandishi wa habari waache kuandika habari zisizo na
ukweli ndani yake kwani wanao athirika na hilo ni wengi. Alisema
uandishi wa habari ni taaluma hivyo wanaoitumikia taaluma hiyo inawapasa
kufanya kazi kwa weledi na kufuata kanuni na taratibu za taaluma hiyo.
Akichangia
hoja ya vijana alisema vijana ni Taifa la leo. Iwapo Serikali itatoa
kipaumbele kwa vijana ajira itapatikana. Hata hivyo aliisifu Serikali
kwa jitihada inazochukua za kusaidia vijana katika mikopo inayo wanyanyua, mpango mkakati wa maendeleo ya vijana ni moja ya njia ya kuinua vijana nchini.
Post a Comment