Baadhi ya majeruhi wakiwa wameanguka chini kufuatia
shambulio la bomu lililofanywa na mtu asiyejulikana ambapo zaidi ya watu 40
wamejeruhiwa na wengine watatu hali yao ni mbaya; tukio hilo lilitokea katika
ibada ya uzinduzi wa kanisa la Mtakatifu Joseph lililoko kata ya
Olasiti, mkoani Arusha jana.Picha na Ferdinand Shayo
--
Takriban
watu watatu wamekufa kwenye mripuko wa bomu Jumapili asubuhi katika
kanisa Katoliki la Olasiti nje kidogo ya mji wa Arusha, Tanzania.
Kwa
mujibu wa Padri Festus Mangwangi ambaye ni paroko msaidizi wa kanisa
katoliki jimbo la Arusha, mripuko ulipotokea walikuwa tayari kubariki
maji kwa ajili ya uzinduzi wa kanisa, shughuli iliyokuwa ikiongozwa na
balozi wa Papa Francis.Wengine kadhaa walijeruhiwa huku balozi wa papa
na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalumu ya kuzindua parokia
mpya ya mtakatifu Yosefu walinusurika.
Hata
hivyo Padre Mangwangi ameiambia BBC kuwa taarifa walizonazo muda mfupi
baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali, kuna watu watatu kati yao
waliofariki na wengine wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Mount
Meru mjini Arusha.
Taarifa moja inasema watu kama 80
walijeruhiwa.Watalaalamu wa miripuko na polisi wanaendelea na uchunguzi
kuhusiana na mlipuko huo.Bado hakuna taarifa ya chanzo cha mripuko au
kama kuna mtu au kundi lilohusika.
Lakini msemaji wa polisi alieleza kwamba wanashuku kuwa mripuko ulisababishwa na bomu.Hili
ni shambaulio la kwanza la bomu nchini Tanzania japokuwa mwaka huu pia
kulikuwa na tukio la mauaji ya Padre wa kanisa hilo visiwani Zanzibar,
ambaye alipigwa risasi wakati akiwa anajiandaa kuingia .
1 comments:
FREEMASON WATAENDELEA KUNYWA DAMU ZA WATANZANIA HIMA REDIO SAFINA KEMEENI HUYU SHETANI ALIYEJENGA KIOTA HAPO ARUSHA WANAABISHA HUO MJI WENYE UPAKO ULIOOKOA WENGI AU NABII HAKUBALIKI KWAO
ReplyPost a Comment