Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na mbunge wa kuteuliwa James Mbatia
--
Mwenyekiti wa chama Cha NCCR-Mageuzi katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Kenned
Staford Festo amejitoa katika uongozi wa chama hicho kwa madai kuwa
chama hicho kimekosa mwelekeo katika kuwahamasisha wanachama na wananchi
kwa ujumla kuondoa changamoto zao katika kujipatia maendeleo wilayani
humo.
Mwenyekiti huyo amechukua uamuzi huo jana baada ya
kamati tendaji ya chama hicho mkoani Kagera kumsimamisha kwa muda wa
miezi miwili iliyopita tangu Februari 20 mwaka huu ikidaiwa alishiriki
maadhimisho ya miaka 36 ya CCM wilayani Ngara.
Akitangaza kujiuzulu Mei 2, Staford alisema
amechoka kutumikia chama kisicho na ruzuku ya kuchangia maendeleo na
ametumia gharama nyingi kuwahudumia wanachama huku akikosa nguvu kutoka
kwa viongozi ngazi ya taifa akiwamo Katibu wa Chama hicho Taifa, Samweli
Ruhuza. (Shaaban Ndyamukama)
Post a Comment