Na Beatrice Mlyansi Maelezo
WAZIRI wa ulinzi na Jeshi la kujengaTaifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha amewataka viongozi wa dini nchini kuwa makini na kauli wanazotoa kwa waamini wao kwani zinaweza kuleta madhara makubwa.
Nahodha ameyasema hayo jana jijini Dar es saam katika kongamano la siku mbili na viongozi wa dini ili kujadili mstakabali wa ulinzi na usalama nchini.
Waziri Nahodha ameeleza kuwa kuwepo kwa dini mbili za Kikristo na Kiislamu sio mzigo bali kauli zinazotolewa na viongozi wa dini hizo kusema vibaya dini nyingine ndio tatizo.
“Kuwepo kwa dini hizi mbili hakuwezi kuwa mzigo,tatizo ninaloliona ni kauli zinazotolewa na abaadhi ya viongozi, inabidi tuwe makini na wa kweli maana wakati mwingine matendo yanasema zaidi”.Alisema waziri Nahodha.
Alisema viongozi hao wanatakiwa kuwa makini sana kwani kauli moja inaweza kutafsiriwa vibaya na upande mwingine bila kukusudia au la.
Waziri ametaka viongozi hao wadini wajifunze kupitia waasisi wa imani zao Bwana Yesu Kristo na Mtume Muhamad ambao walifundisha bila kukashifu imani nyingine pamoja na mwanafalsafa Confucias ambaye alisisitiza watu mwenye busara kutobadili misimamo yao kwenye masuala yenye maslahi ya muda mrefu.
Post a Comment