Mwenyekiti
wa Chama cha Wabunge wanawake Bungeni (TWGP) . Mhe. Anna Abdallah (Mb)
akifungua rasmi semina hiyo siku moja kuhusu namna bora ya uwasilishaji
wa Miswada binafsi na hoja Binafisi Bungeni kwa wabunge wanawake.
Kushoto ni katibu wa chama hicho Mhe. Angela kairuki na aliyekulia ni
Makamu Mwenyekiti Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa.
Mtoa
mada kutoka Ofisi ya Mshauri Mkuu wa mambo ya Sheria wa Bunge Ndg.
Matamusi Fungo akiwasilisha mada kwa wabunge wanawake kuhusu
uwasilishwaji wa Miswada ya Serikali Bungeni.
Bi.
Stella Bwimbo nae kutoka Ofisi ya Mshauri Mkuu wa mambo ya Sheria wa
Bunge akiwasilisha mada kuhusu uwasilishwaji wa Miswada binafsi ya
sheria Bungeni.
Ndg.
Mosi Lukuvi kutoka Ofisi ya Mshauri Mkuu wa mambo ya Sheria wa Bunge
akiwasilisha mada kuhusu uwasilishwaji wa Hoja binafsi Bungeni kwa
waheshimiwa wabunge wanawake.
Katibu
wa Chama cha Wabunge wanawake Bungeni Mhe. Angela kairuki akikaribisha
michango kwa waheshimiwa wabunge mara baada ya kusikiliza mada. Kushoto
ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa.
Mbunge wa viti Maalum (CCM) Diana Chilolo akiuliza swali kwa mtoa mada.
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe. Cecilia Paresso akiuliza swali kwa watoa mada.
Mbunge wa viti Maalum (CCM) Devota Likokola nae akichangia.
Mbunge wa viti Maalum (CCM) Maria Hewa akitoa mawazo yake.
*********
Chama
cha Wabunge wanawake katika Bunge la Tanzania (TWGP) leo wamefanya
semina ya siku moja kwa wabunge wote wanawake kwa lengo la kuongeza
uelewa mpana katika namna bora ya uwasilishaji Miswada au hoja binafsi
Bungeni.
Akifungua
semina hiyo, Mwenyekiti wa chama hicho cha Wabunge wanawake Bungeni.
Mhe. Anna Abdallah amewataka wabunge wanawake wote bila kujali vyama
vyao kuhakikisha wanaitumia vizuri Ofisi ya mshauri mkuu wa mambo ya
sheria wa Bunge katika kuwasilisha Miswada au hoja Binafisi.
Amesema
wabunge wanawake wanawajibu wa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi
hususani wanawake nchini ikiwa ni pamoja na kuleta hoja au miswada
Bungeni yenye kulenga kuifanya serikali iweze kutatua kero
zinazowakabili wananchi wake.
“Waheshimiwa
wabunge, pamoja na kwamba mimi nikipindi changu cha nane hivi sasa bado
kuna mwamko mdogo kwa waheshimiwa wabunge wanawake kuleta miswada au
hoja binafsi bungeni. Naamini tukiitumia vizuri Ofisi hii pale
tutakapokuwa tuna mawazo yetu, watatusaidia sana kutuandalia hoja
binafisi au miswada kulingana na matakwa yaliyopo ya kikanuni”alisema
Mhe. Anna Abdallah
wakichangia
mada zilizowasilishwa hapo, wabunge wengi wanawake wameomba kuwe na
utaratibu mzuri wa kuhakikisha kuwa kila mara elimu hii inatolewa kwa
lengo la kujikumbusha baadhi ya taratibu za kikanuni na hata kisheria
katika uwasilishaji wa hoja binafsi na miswada binafsi Bungeni.
“Kuna
haja ya kuwa na semina katika maswala haya angalau mara moja kila wakati
wa vikao vya Bunge ili kujikumbusha mambo kadhaa yanayotawala katika
uwasilishwaji wa miswada binafsi au hoja Binafsi mwenyekiti kwa kuwa
tuna mambo mengi tungependa kuyaleta Bungeni kupata baraka zake. Kwa
kujikumbusha na mambo haya tutaiva kwelikweli katika kuwawakilisha
wananchi wetu mwenyekiti”. Alichangia Mhe. Anne Kilango Malecela.
Jumla
ya mada tatu ziliwasilishwa katika Semina hiyo iliyoandaliwa na chama
hicho cha wabunge wanawake Bungeni (TWGP) kwa kushirikiana na Ofisi ya
msahuri wa maswala ya sheria wa Bunge ambazo zote zililenga kuwapa
uelewa wabunge kuhusu namna bora na mambo ya kuzingatia wakati wa
kuwasilisha miswada binafsi na hoja binafsi Bungeni kwa wabunge
wanawake.
Credits: Issamichuzi matukio
Post a Comment