Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma akizungumza na wanahabari
Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bw. Aman Mwamwindi
..................................................................................................................................
SERIKALI mkoa wa Iringa imekanusha
vikali taarifa zinazoenezwa na machinga mjini Iringa kuwa
mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi
kuruhusu machinga kuendelea na biashara jumapili katika eneo hilo
la Mashine tatu ambalo kisheria limepigwa marufuku.
Hatua ya kumtafuta mkuu wa mkoa wa Iringa kwa njia ya simu
usiku huu ili kuelezea hatua hiyo ya kuwepo kwa uvumi wa
machinga kuruhusiwa kufanya biashara ,mkuu huyo wa mkoa amesema
hakuna ruhusa iliyotolewa ya kuendelea kwa biashara kwa machinga hao.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa kikao
cha meya na wafanyabiashara kililenga kujadiliana eneo rafiki la
wao kufanyia kazi na sio kikao kilichoruhusu machinga hao
kuendelea na kazi eneo hilo .
" Meya alichowaambia machinga hao ni kuendelea kuwepo eneo la mashine tatu wakati suala lao linafanyiwa kazi"
CREDITS: mtandao wa www.matukiodaima.com
Post a Comment