Mahmoud Ahmad Singida
Walemavu hapa nchini hasa viziwi wametakiwa kutoogopa kwenda kupata huduma ya matibabu ya Fistula kwani matibabu hayo yanatolewa bure kwenye vituo vyote vya Afya hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Katibu mtendaji wa taasisi ya maendeleo kwa viziwi Tanzania(TAMAVITA)Bw.Kelvin Nyema wakati akiongea na waandishi wa Habari kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida na kuwataka kutoogopa kwenda kutibiwa ugonjwa huo.
Nyema aliwataka Viziwi hapa nchini kutojificha kwa madai yakutokuwa na hela kwani ugonjwa wa Fistula unatibiwa bure kwenye vituo vyote vya Afya na kuwa wapo kuhamasisha wenzao kwenye vijiji kwenda kutibiwa ugonjwa huo.
“Unajua viziwi wengi hujificha wanapoumwa na uugonjwa wa fistula wakidai kuwa hawana hela ya kulipia matibabu hivyo tupo hapa kuhamasisha wenzetu wakatibiwe ugonjwa huo”alisema Nyema.
Nyema alisema kuwa ugonjwa wa fistula huwakumba wanawake nchini na kuwa wao (TAMAVITA)wakishirikiana na wizara ya Afya na ustawi wa jamii kupitia Idara ya kinga wamejikita kutoa elimu kwa jamii hiyo ya pembezoni kujua umuhimu wa kujali afya zao.
“Tumedhamiria kuwapatia elimu ya ugonjwa wa fistula walemavu kwa kujikita kwenye vijiji na mijini waweze kupata huduma hii kwani wao wanadhani matibabu ni fedha wengi wao husema kuwa hawana fedha ya matibabu na kuishia kuumia na ugonjwa huo”alisema Nyema.
Ibainika kuwa mkoa wa Singida unawanawake wengi wanaougua ugonjwa wa fistula ndiyo maana nasi tumekuja mkoani hapa kuendesha kampeni ya fistula kwa wakinamama walemavu wa kusikia ili waweze kutibiwa.
Wakati huo huo Mkuu wa wilaya mwalimu Queen Mlonzi ametoa kauli katika kampeni iliyoendeshwa na Vodacom na hospitali ya CCBRT ambayo imelenga katika uhamasishaji wa kinamama kujitokeza kutibiwa ugonjwa huo baada ya kubainika kuwa mkoa wa SINGIDA ni miongoni mwa mikoa yenye wakinamama wanaougua ugonjwa wa fistula.
Katika kuhakikisha kuwa wanawake wanougua ugonjwa huo wanapata fursa ya kutibiwa bila malipo kampuni ya VODACOM imetoa kiasi cha shilingi bilioni nane kugharamia matibabu kwa wakinamama waougua FISTULA ,kama anavyoeleza mwakilishi wa VODACOM ,Salimu Mwalimu
Baadhi ya wakinamama na wakina baba ambao wake zao wamepata matibabu na kupona wametoa ushuhuda wao katika kampeni hizo
Mwakilishi toka hospitali hiyo ya CCBRT amesema tatizo la ugonjwa huo hapa nchini ni kubwa lakini wakinamama wengi hajapata taarifa za kutosha kuhusiana na matibabu
Post a Comment