*NI KWA AJILI YA KUSAIDIA AFYA YA MAMA NA MTOTO TANZANIA
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete (katikati) akisalimina na
Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhavile na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Montage Limited, Teddy Mapunda.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Salma Kikwete (kulia)
akizungumza na Uongozi wa Montage pamoja na wadhamini wa Harambee
iliyoongozwa na Kampuni ya Montage kwaajili ya kuchangisha fedha
kwaajili ya kusaidia matibabu ya Mama na Mtoto nchini Tanzania.
Mkurugenzi
wa ITV, Joyce Mhavile (kushoto)akizungumza jambo na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Montage Limited, Teddy Mapunda kabla ya kukabidhi hundi kwa
Uongozi wa WAMA.
Mke wa Rais
na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Salma Kikwete
akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 70 kutoka kwa
Mkurugenzi wa Montage Limited, Teddy Mapunda ikiwa ni mchango wa kampuni
hiyo katika kuchangia Afya ya Mama na Mtoto. Fedha hizo ni sehemu ya
michango ya wadau mbalimbali iliyopatikana katika harambee maalum
iliyopendeshwa na Montage hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa
Fedha wa Montage, Zainabu Mkindi (wapili kushoto)na kulia ni Katibu wa
WAMA, Daud Nassib. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.
Post a Comment