Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii kupitia Tangazo lake kwenye Gazeti la Habari
Leo la tarehe 20 Aprili, 2013 siku
ya Jumamosi na la tarehe 23 Aprili, 2013 siku ya Jumanne na kwenye tovuti ya Wizara,
ilitangaza nafasi mbalimbali za kazi za
Kada ya Afya zikiwemo za Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii
Wasaidizi, Walezi wa Watoto, Maafisa Lishe na Maafisa Lishe Wasaidizi.
Wizara inapenda kuwajulisha waombaji wa
nafasi za Kada tajwa hapo juu zitashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti
ya Ajira.
Hivyo, waombaji wote waliotuma maombi yao
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wanajulishwa kuwa maombi yao yatapelekwa Sekretarieti ya Ajira kwa ajili ya
uchambuzi na usaili.
Tangazo hili halihusu waombaji walioomba Kada
mbalimbali za Afya ambazo zitashughulikiwa moja kwa moja na Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii.
Kaimu Katibu Mkuu
WIZARA YA
AFYA NA USTAWI WA JAMII
22 Mei, 2013
Post a Comment