Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

YOA YAJIPANGA KUTOA TUZO KWA VIJANA KUANGALIA VIPAUMBELE MBALIMBALI

 

  
a-grouphoto
Na Hassan Silayo – MAELEZO
 SHIRIKA la Vijana wa Afrika (YOA) lenye makao yake jijini Dar es Salaam, linaandaa tuzo kwa ajili ya vijana walio chini ya umri wa miaka 30
 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bwana Awadh Milasi wakati akiongea na waandishi wahabari  leo(jana) jijini Dar es Salaam.
Awadh alisema kuwa tuzo hizo zitatokana vipaumbele nane ambavyo ni Habari,Ujasiriamali,Uvumbuzi,
Mitindo ya mavazi,Michezo,Sanaa na Ubunifu,Burudani na Mchango kwa jamii ambayo ndiyo tuzo kuu.
 Alisema kuwa lengo  kuandaa tuzo hizo ni kuleta fikra chanya kwa vijana wengi wa kitanzania  ili kuibua vipaji na kupambana  na changamoto hili kuletea maendeleo.

 Aidha aliongeza kuwa mchakato wa mapendekezo ya majina ya washiriki uko wazi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 16 na 30
“Shilikaa linapenda kufahamisha umma na vyombo vya habari kuwa mapendekezo sasa yapo wazi kwa vijana wa kitanzania wenye umri kati ya miaka 16 na 30 kwa kuzingatia vigezo vilivyoainishwa” Alisema Awadh.
Kwa upande wake Afisa Rasilimali Fedha,Mushumba Avitus ameeleza nia yao ni kushawishi na kutoa mchango kwa Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutambua uwepo wa shughuli muhimu zinazofanywa na vijana katika jamii
 Mshumba amesema vijana wenye uthubutu ni wakati wao wa kujitokeza na kushiriki katika tuzo hizi ambapo alisema kuwa washiriki watapendekezwa kupitia tovuti ya www.youthawards.or.tz  ulionza tarehe 2 Mei hadi tarehe 7 Juni 2013.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top