Naibu
Waziri wa Katiba na sheria, Mhe. Anjela Kairuki, amezindua rasmi,
Ilani ya Madai ya wanawake kwenye Katiba mpya leo katika viwanja vya
mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).
********
Naibu waziri
amewataka wanwake kukataa kutumika na wanasiasa kama daraja la
kuwapistisha wao kushika madaraka. “ninawataka wanawake tukatae
kutumika, hata sisi tunaweza, tumetumiwa sana kupitisha mambo ya watu
wengine, waoa wananufaika sisi tuabaiki kulalamika, umefika wakati na
sisi tutumie fursa zilizopo kuhakikisha tunanufaika nazo na kupata
naafsi ya ushiriki wa kutosha kwenye uongozi” amesema Kairuki
Ameongeza kuwa
wanwake wajitahidi kujitokeza katika kugombea nafasi za uongozi katika
ngazi mbalimbali za uongozi na kuytumia mchakato wa Katiba mpya kama
fursa ya kupata nafasi za kutosha kwenye uongozi, “Tusipoutumia huu
mchakato kupata nafasi, tutajuta, kwa kipindi kirefu kumekuwepo na
malalamiko kuwa hatupewi nafasi, lakini huu mchakato wa Katiba unapita
lazima tuutumie kufanikisha ajenda zetu wanawake na kuunganisha nguvu za
pamopja katika kudai mgawanyo sawa wwa rasilimali za taifa hil”
Mhe. Kairuki amewataka wanawake kuhakikisha wanaungana na kutokukubali kugawanywa au kujigawa kimakundi.
Amesema kuwa
kila mwanamke ajitahidi kuisoma ilani ya madai iliyoandaliwa na TGNP ili
kubeba agenda za wanawake kwenye mijadala inayoendela ya kujadili
rasimu ya katiba kwenye mabaraza ya katiba mara yatakapoanza.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TGNP Ussu Mallya alisema TGNP kwa kushirikiana na
wanaharakati wa masuala ya ukombozi wa wanawake, usawa wa kijinsia, haki
za Binadamu, utawala bora na Maendeleo wamekuwa na utaratibu wa kuandaa
ilani mbalimbali za wananchi kuanzia uchaguzi wa mwaka 2000, 2005 na
2010.
“Mwaka huu
tumeandaa Ilani ya madai ya wanawake wa Tanzania kwenye katiba mpya, ili
kuwezesha jamii kuchambua, kujadili na kuangalia maeneo muhimu ya kudai
uwajibikaji na utekelezaji wakati wa mijadala ya kuandaa katiba mpya.
Alisema mchakato
wa kuandaa madai ya katiba mpya umetokana na ushiriki mkubwa wa wadau
mbalimbali yakiwemo mashirika katika ngazi ya kitaifa na jamii
yanayotetea haki za Binadamu, jinsia na maendeleo, Femact na GDSS ambazo
hufanyika kila Jumatano mabibo.
Kwa mujibu wa Mallya alisema madai
hayo yametokana na ushiriki na sauti mbalimbali za wadau wanaotetea
haki za wanawake na hususani haki zao za kikatiba na kuongeza kuwa ni
matumaini yao kuwa tume ya mabadiliko ya katiba inatambua changamoto
zinazowakabili wanawake ili yaweze kuingizwa katika katiba mpya.



Post a Comment