Na Mwandishi Wetu, Arusha
KUTOKANA
na mlipuko wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu, uchaguzi wa Kata nne jijini
Arusha uliopangwa kufanyika leo umeahirishwa na kupangwa tena kufanyika Juni 30
mwaka huu.
Mlipuko
uliotokea jana jijini Arusha, ndivyo ilivyoleta hali hiyo ya kumwaga
damu.
Uchaguzi
huo umeahirishwa huku mlipuko wa jana ambao ulitokea wakati Mwenyekiti wa Chama
Cha Demokrasia na Maeendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anafunga mkutano wake,
ulisababisha kuzuka kwa taharuki kubwa katika mkutano huo wa
kampeni.
Watu kadhaa wamehofiwa kufa katika mlipuko huo, ambao umezidi kuomnyesha kuwa hali ya amani kataika Taifa hili la Tanzania inazidi kutoweka.
Mwandishi
wetu jijini Arusha, alisema kuwa uchaguzi huo umeahirishwa. Bado
tunafuatilia kwa kina mtifuano huo sambamba na hali za majeruhi na waliopoteza
maisha.
Mlipuko
huo ulitokea na kuleta wasiwasi mkubwa katika kazi za kijamii, kama vile
mikutano na makongamano pale yanapohusisha watu wengi na kuleta hofu kubwa.
Post a Comment