Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na
Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
Salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete.
Mechi
hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi
atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha
fedha za ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila
aina, sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji
huo.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye
pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku
mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya
kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi
hiyo ya aina yake.
Alisema
kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo
wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya
wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya
wabunge.
“Tupo
imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya
wote waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu
wa Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
“Katika
mechi hizi, mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen
Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.
Aliwataja
Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas
Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin
Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman
Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya
Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza
Mwamlima (Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela
(Arusha), Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo
(Korogwe), uhingo rweyemamu handeni, Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima
(Bariadi), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela
Rubinga (Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni
msemaji wa timu hiyo.
Aidha,
Muhingo alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi),
Sarah Dumba (Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni
Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula
(Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha
(Urambo) Jacqueline Liana ( Magu).
Post a Comment