Balozi
Seif akikata keki iliyoandaliwa na Uongozi wa Tamsa kwa ajili ya
kunadiwa kwenye Mkutano huo ili kutunisha mfuko wa Chama hicho
akishuhudiwa na Rais wa Chama hicho Bwana Biswalo Yango pamoja na baadhi
ya wanachama wenzake.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiingia ndani ya
ukumbi wa Mbwezi Beach Motel Royal Skyline Jijiji Dar es salaam
kuufungua Mkutano wa kwanza wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania
(TAMSA)
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiufunguwa Mkutano wa kwanza
wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania TAMSA hapo Mbezi Beach
Royal Skyline Jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiufunguwa Mkutano wa kwanza
wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari Tanzania TAMSA hapo Mbezi Beach
Royal Skyline Jijini Dar es salaam.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chama cha Wafafunzi wa
Udaktari Tanzania Tamsa mara baada ya kuufungua Mkutano wao wa kwanza
hapo Mbezi Beach Royal Skyline Jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Wanahabari mara
baada ya kuufunguwa Mkutano wa kwanza wa Chama cha Wanafunzi wa Udaktari
Tanzania (Tamsa) hapo mbezi beach.
Uongozi
wa Juu wa Chama cha Wanafunzi wa udaktari Tanzania Tanzania { TAMSA }
ukimsindikiza Balozi Seif mara baada ya kukamilika kwa ufunguzi wa
Mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya Mbezi Beach Royal Skyline
Jijini Dar es salaam. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
***************************************
Juhudi
za Madaktari katika kuzingatia utekelezaji wa majukumu yao ya kazi ya
kila siku kupitia msingi wa maadili uliowekwa katika fani hiyo ndio njia
pekee itakayoendelea kuleta faraja miongoni mwa Wagonjwa pamoja na
Wananachi wakati wanapohitaji kupatiwa huduma za afya.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo katika
dhifa maalum ya uzinduzi wa Mkutano wa kwanza wa Chama cha wanafunzi
Madaktari Tanzania { TAMSA } uliofanyika katika ukumbi wa Mbezi Motel
Royal Skyline Jijini Dar es salaam.
Balozi
Seif alisema wananchi wamekuwa wakiwalalamikia baadhi ya Madaktari
na watendaji wa sekta ya Afya kutokana na huduma wanazotoa ambazo wakati
mwengine huambatana na jeuri na dharau jambo ambalo linakwenda kinyume
na maadili yao.
Alisema
imani ya wananchi ni vyema ikarejeshwa na baadhi ya watendaji wenye
tabia hiyo kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa wakielewa kwamba
jukumu walilolibeba ni kazi ya wito inayohitaji hekma, ustahamilivu na
uvumilivu.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wanachama wa Chama hicho cha
Wanafunzi Madaktari Tanzania { TAMSA } kwa juhudi zao za kuanzisha
Taasisi hiyo yenye lengo la kuunganisha nguvu za pamoja za Madaktari
hao.
Aliwahahikishia
Wanachama hao kwamba Serikali zote mbili zitahakikisha kuunga mkono
jitihada zao katika kuwapatia msaada unaostahiki zikiwemo fursa za
masomo ya Juu katika ngazi ya Madaktari Mabingwa.
Balozi
Seif alieleza kwamba Sera za Serikali zote ni kuimarisha miundo mbinu
itakayowezesha kuwepo kwa kituo cha Afya kila baada ya kilo mita Tano
ili kuwaondoshea usumbufu wa huduma za afya wanachi hasa katika maeneo
ya Vijiji.
Aliwaasa
wanachama hao kujiepusha na migomo kwa kisingizio cha kutumia haki yao
ya kidemokrasia katika kushinikiza madai au malalamiko yao kitendo
ambacho huleta bughdha kwa wagonjwa na wakati mwengine kutishia
kuhatarisha maisha yao.
Alieleza
kwamba Serikali imekuwa ikitumia nguvu na gharama kubwa katika
kuwaandaa madaktari kwa lengo la wamalizapo mafunzo waweze kutoa huduma
kwa Umma Kitaalamu na kwa ufanisi zaidi.
“
Moja kati ya jambo ambalo Serikali isingependelea kuliona linaonekana
ni migomo ambayo kwa kweli huleta fadhaa na wakati mwengine kuhatarisha
maisha miongoni mwa wananchi “ Alisisitiza Balozi Seif.
Mapema
Rais wa Chama cha Wanafunzi Madaktari Tanzania { TAMSA } Bwana Biswalo
Yango aliipongeza Serikali Kuu kwa juhudi zake za kuunga mkono makundi
mbali mbali ya Jamii hapa Nchini kikiwemo chama chao.
Hata
hivyo Bwana Yango alisema Sekta ya Afya bado inaendelea kukabiliwa na
changamoto kadhaa ambazo alizieleza kwamba ana imani kuwa zinaweza
kutatulika kwa kutumia njia ya ushirikiano wa pamoja kati ya Serikali
na wadau wa sekta hiyo.
Uzinduzi
wa Mkutano huo wa kwanza wa Chama cha Wanafunzi Madaktari Tanzania {
TAMSA } ulijumuisha mada tatu ikiwemo Historia ya Tamsa tokea kuanzishwa
kwake.
Washiriki
wa Mkutano huo pia walipata fursa ya kushiriki zoezi maalum la ununuzi
wa keki pamoja na T. Shirt lililoongozwa na mgeni rasmi Balozi Seif kwa
lengo la kusaidia kutunisha mfuko wa Chama hicho.
Wanachama
wa Chama hicho kilichoanzishwa karibu miaka mitano iliyopita wanatoka
katika vyuo Vikuu vya Afya Moi Muhimbili, Kairuki pamoja na
International Medical Technolodge.
Credit: Mafoto blog









Post a Comment