Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BENKI YA DUNIA NA DANIDA WATATHIMINI MRADI WA UENDELEZAJI MIJI (TSCP) NA KUENDELEZA HISANI

 


_DSC0166
UJENZI WA STANDI YA MABASI MAKUBWA DODOMAUKIENDELEA, UJENZI HUU UNAOFANYWA NA MRADI WA UENDELEZAJI MIJI WA TSCP, ULIO CHINI YA OFISI YA WAZIRI MKUU – TAMISEMI DSC00716 DSC00727
Na Mboza Lwandiko (OWM-TAMISEMI)
Mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TSCP), ambao upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) ambao ulizinduliwa rasmi 2010, umedhihirisha jinsi ulivyoshamiri kwa kiwango kikubwa. Mabadiliko makubwa yameshaanza kuonekana katika Miji 7 ambamo Mradi huu unaendelea na shughuli zake. Mikoa hii ni; Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Mbeya, Tanga na Kigoma Haya yalibainishwa hivi karibuni wakati wa Kikao cha kutathimini utekelezaji wa Tscp kilichofanyika Dodoma Hoteli – Dodoma.
Kikao hicho kilikusanya wajumbe wa Benki ya Dunia, DANIDA, OWM-TAMISEMI na wawakilishi wa Halmashauri kwa kusudi la kutathimini kama Mradi huo unaendelea vyema kufanya ipaswavyo au la. Pia kubaini kama matakwa ya mipango ya Mradi yanafanikiwa na kutoa ushauri ambao utasaidia kufanikisha mafanikio ya kutimiza makusudi ya Mradi kama inavyotarajiwa.
Tscp inafadhiliwa na Benki ya Dunia na DANIDA; Jumla ya gharama zilizotolewa ni Dola za Kimarekani Milioni 175.5, ambapo Milioni 163.2 ni kutoka Benki ya Dunia na Milioni 12.2 ni kutoka DANIDA.

Kabla ya Kikao cha kutathimini Tscp kwa ujula, Timu kutoka Benki ya Dunia, DANIDA na  Wawakilishi wa Tscp walitembelea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mradi katika Miji ya Arusha, Mwanza, Mtwara na Mbeya ili kujionea kikamilifu yale yaliyotekelezwa katika maeneo hayo.
Wakiwa katika Mji wa Mwanza, Mtaalam wa Mazingira wa Benki ya Dunia; Jane Kibassa aliwataka wawakilishi wa Tscp – Mwanza kuwa makini katika kuhakikisha usafi wa daraja na mifereji ili kuepukana na tatizo la kuziba kwa mifereji kwa uchafu, pamoja na kuepukana na magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na uchafu. Vile vile mshauri wa Kimataifa wa Tscp, Linda Skoog’s alisisitizia kutunzwa vyema kwa vifaa vya mfumo wa habari za kijiografia(GIS).
Wakati akitoa hotuba yake katika Kikao cha Kutathimini Utekelezaji wa Tscp, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Mhe. Aggrey Mwanri alisema kwamba kwa ujumla kazi ya Utekelezaji wa Tscp unaridhisha.
Kwa upande wa Mtaalam wa Miji wa Benki ya Dunia,World, Andre Bald alihimiza umuhimu wa kuzingatia maboresho katika maeneo yaliyoonekana kuwa na udhaifu katika Miji yote 7. Aidha alipongeza sana Mji wa Arusha kwa kuonekana kufanya kazi  saba yake vizuri sana na kuitaka Miji mingine 6 kuiga mfano kutoka kwa Mji wa Arusha.
Kabla ya kumalizika kwa Kikao hicho. Wafadhili na wajumbe wengine wa kikao walitembelea shughuli mbalimbali za Mradi zilizomo Dodoma Manispaa na CDA. Wakitembelea maeneo hayo. Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Onur Ozlu alisema; “ Amefurahishwa na barabara zilizo na maeneo maalum ya wapiti kwa miguu. kwakuwa ni hatari sana kwa watu kutembea katika barabara pamoja na magari, baiskeli na pikipiki”. Naye Kaimu Katibu Katibu Mkuu, OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini akitembelea eneo la Kisasa alisema; “ Hakuna mashaka kwamba eneo hili limekuwa na mtazamo mpya kabisa ukilinganisha na miaka miwili tu iliyopita”.
Arusha, Maendeleo makubwa yamejitokeza pia; Kwa barabara, msongamano wa magari umepunguzwa, kwa marekebisho ya barabara za mijini, kwenye maeneo yaliyofanyika karibu na eneo la biashara, ambapo barabara hizo zilizokuwa katika hali mbaya. Sasa barabara hizo zimewekewa lami, zina taa za barabarani na mifereji ya kudumu ya maji pembezoni mwa barabara hizo.
Sasa Manispaa ya Arusha imeunganisha barabara nyingine ambazo zitasaidia kupunguza msongamano wa Magari katikati ya Mji. Barabara hizo ni pamoja na barabara ya Majengo-Bumico (inayounganisha barabara ya Dodoma na Arusha-Namanga, ambapo standi ya basi ya sasa, itahamishwa, na barabara ya Col. Ndomba (itaunganisha barabara ya Njiro na Engira) na kuendeleza ile ya Njiro.
Kwa kigoma, shughuli ambazo zinatekelezwa na mradi, zilikuwa pamoja na; Ujenzi wa barabara, ujenzi wa madaraja, ujenzi wa standi za mabasi na malori na ujenzi wa dampo. Mabadiliko makubwa ya kupendeza yameonekana zaidi kwenye standi za mabasi.
Benki ya Dunia imechangia tena kwenye miradi mingine ya kuendeleza Miji Tanzania, ambapo Miradi hiyo inategemewa kufanyika katika maeneo mengine yote ambayo haikuwa na mradi wa tscp. Mradi huo unajulikana kama; The Urban Local Government Strengthening Programme – (ULGSP).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top