Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
INAHITAJI
akili ya kiuwendawazimu kupita huku na kule kusifia mwendelezo mbovu wa siasa za
Tanzania, hasa baadhi ya vyama vya upinzani kufanya mambo ya
kijinga.
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe
Ni
pale mwanasiasa anayejiona anakubalika kwa wananchi wake, anaamua kwa makusudi
kuvunja sheria za nchi. Huu ni ujinga. Unahitaji kupingwa vikali na kila
muhibiri wa amani.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania, Jakaya
Mrisho Kikwete.
Kwa
wiki moja sasa, jiji la Arusha limekuwa likitawaliwa na uvunjifu wa amani,
taharuki na kusababisha matatizo makubwa. Tangu siku ya Jumamosi ya Juni 15,
wananchi wa Arusha wamekuwa wakiendelea kuishi kwa mashaka na wasiwasi
mkubwa.
Watu
watatu wamefariki Dunia, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya, ikiwa ni baada
ya bomu kurushwa katika mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
huku ukihudhuriwa pia na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.
Ikumbukwe
kuwa, matokeo ya ghasia jijini Arusha si mara ya kwanza, maana kila siku
kunakuwa na mgogoro mkubwa na kuwaacha Watanzania wenzetu wakiwa hawaelewi cha
kufanya.
Mara
baada ya kutokea mlipuko huo, Mbowe, kama mwenyekiti wa Chadema, alitangaza
kuwazuia wabunge wote wa chama hicho kuingia kwenye vikao vya
Bunge.
Ni
kauli tata sana kwa maendeleo ya Taifa. Taifa ambalo, linahitaji bajeti bora
yenye maslahi na Watanzania wote. Lakini kuzuia wabunge kuhudhuria vikao vya
Bunge, ni vitendo vya kushangaza mno.
Kwa
mujibu wa Mbowe, aliwazuia wabunge kuhudhuria vikao vya Bajeti ili washiriki
kwenye misiba ya waliokufa kutokana na mlipuko huo wa Soweto, jijini
Arusha.
Mbowe
anatangaza hatua hii huku akijua kuwa Chadema haipo Arusha peke yake. Chadema
pia inahitaji kura za wananchi wote, kama vile Tanga, Kilimanjaro, Mwanza,
Mbeya, Morogoro, Iringa na mikoa mingine kama kweli inahitaji kushika
dola.
Lakini
Chadema wao wameonekana kuweka nguvu kubwa kwa jiji la Arusha, tena wakifikia
hata kuvunja sheria za nchi. Ndio hapo ninapoanza kujiuliza juu ya mwendo
huu.
Tunahitaji
viongozi wendawazimu. Wale wanaoweza kufanya kazi bila kuogopa sura au mihemko
ya viongozi wa vyama vya siasa. Kwa mfano, sheria inajieleza juu ya vyama vya
siasa vinavyofanya vitendo vya vurugu na adhabu yake pia.
Tunahitaji
sasa serikali kwa kupitia Msajili wa Vyama vya siasa, John Tendwa kuwa makini
zaidi. Jeshi la Polisi nalo lihakikishe kuwa linasimamia vyema usalama wa
raia.
Usalama
ambao mara kadhaa umekuwa hatarini kwasababu ya matakwa ya viongozi wachache wa
kisiasa. Huu ndio ukweli. Jeshi la Polisi Tanzania, mkoani Arusha lilizuia
mikusanyiko isiyokuwa na sababu.
Ili
kuonyesha kuwa Chadema wana lengo lao binafsi, waliamua kufanya mkutano bila
hata kupewa kibali cha polisi. Hapa Chadema walitegemea kitu gani?
Wanataka
waendelee kuvunja sheria wakijua wanaogopwa, hawawezi kuchukuliwa hatua za aina
yoyote? Kila mara wabunge wa Chadema wanafanya vitendo visivyokuwa vya
kiungwana.
Mbunge
kama vile Godbless Lema, Tundu Lissu, Mbowe, Mchungaji Peter Msigwa wamekuwa
wakijifanya wao ndio kila kitu katika Taifa hili, jambo linaloibua maswali kede
kede.
Kuheshimika
kwao wanakuchukulia vibaya, ndio maana matamshi yao mara kwa mara hayajengi
jamii bora zaidi ya kuibomoa kadri wanavyojua wao, lengo lao ni kuichafua
serikali iliyopo madarakani, chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hii
sio njia nzuri kamwe. Tanzania inazidi kuingia kwenye migogoro kama hii
kwasababu ya ujinga wa watu wachache, ambao nashawishika kusema kuwa wana uchu
wa madaraka.
Mara
baada ya mlipuko kutoka Jumamosi, Mbowe hakuonyesha kumfahamu mlipuaji huyo,
zaidi ya kuwazuia wabunge kuingia bungeni, akiwamo Zitto Kabwe, ambaye alipaswa
kuwasilisha Bajeti ya Wizara Kivuli ya Fedha na Uchumi.
Lakini
siku moja baadaye, yani Jumapili, Mbowe huyu huyu anatangaza kuwa anamfahamu
vyema mlipuaji wa bomu, akasema ni Polisi. Sasa kama ndio yeye, maana hakuna
anayeweza kufanya uharifu akachekewa, isipokuwa anahitaji kuchukuliwa hatua
kali.
Kauli
ya Mbowe inakwenda sambamba na tamko la serikali Bungeni, kwa kupitia Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, aambaye alionyesha kupigwa na butwaa
jinsi baadhi ya Watanzania wenzetu wanavyopigania kuiharibia sifa nchi
yetu.
Lukuvi
akafika mbali zaidi kwa kusema serikali itatoa Milioni 100 kwa mtu atakayetoa
ushahidi wa wanaofanya vitendo vya kiharifu, kama hivyo vya kulipua mabomu, huku
nikiamini kuwa Mbowe atatoa ushirikiano kwa kumtaja mtu huyo.
Kwa
uelewa wangu na siasa za Tanzania, zenye kila aina ya mihemko, kutoka baadhi ya
vyama upinzani, sidhani kama Chadema wangeweza kumuacha mhalifu, arushe bomu na
kutokomea kusipojulikana.
Chadema
wasingefanya ujinga huu. Wangemng’ang’ania. Kama wanaweza kushindana na polisi
kwa kuwarushia mawe, wakisema ukombozi unakaribia, kwanini wamuache mtu
anayepiga bomu katika mkutano wao wa kampeni?
Hapa
nini kinatengenezwa? Kwa bahati mbaya wale wasiokuwa na uelewa mzuri juu ya
mambo ya kisiasa, wanajikuta wakipumbazwa na janja za aina hiyo kwenye
propaganda za kisiasa. Naweza kusema kuwa Chadema wao wenyewe wanafuga jini,
hivyo walitafutie damu ya kulinywesha, tofauti na ile ya Watanzania inayomwagika
bila sababu za msingi.
Angalia
ajabu hii, mara baada ya bomu kurushwa kwenye mkutano huo, mtu ambaye anadaiwa
kurusha, hakuweza kukamatwa mara moja kwasababu Polisi hawakupewa ushirikiano.
Ni
pale walipoanza kurushiwa mawe na wananchi kwenye tukio hilo, ambalo baadhi yao
wamepoteza maisha. Siasa za aina hii sio mahali pake. Kila mtu mwenye mapenzi
mema na Tanzania ni wakati wake sasa kuwa makini na kuwa mkali
zaidi.
Watanzania
tunadanganywa na wanasiasa ambao wanatumia nguvu kubwa kuiweka nchi kwenye
kisiwa cha umwagaji damu. Wanasiasa wa aina hii wanatafuta kitu
gani?
Hata
kesho wakifanikiwa kunyakua dola, wanataka waongoze watu wa aina gani? Inauma
sana. Katika kuliangalia hili, naona kufanikiwa kwake ni ngumu, maana kwa bahati
mbaya wapo wananchi wanaojifanya hawanazo.
Wanajifanya
wana uchungu zaidi na nchi hii kuliko Baba wa Taifa, ambaye licha ya kuhangaika
kwa mambo mengi, ila leo hii ametangulia mbele za haki.
Wapambanaji
wengi waliohakikisha kuwa mimi na wengine wenye umri wangu wanakuja kuishi
katika nchi hii. Nchi ambayo kutokana na uongozi bora, kuheshimiana na
kupendana, kulisababisha kutapakaa kwa sifa nzuri ya kisiwa cha
amani.
Kisiwa
cha amani ambacho leo hii watu wanataka kugawanywa kwa dini zao, makabila yao na
mikoa wanayotoka. Leo hii jiji la Arusha, lenye sifa kemkem linanuka
damu.
Kila
siku Arusha kimewaka. Kunanini? Nani kasema Arusha ni lazima damu zimwagike? Huu
sio mwendo mzuri hata kidogo. Ni wakati wetu sasa kila mtu kuwa makini na aweke
msimamo.
Kwa
wale wanaopenda mabadiliko ya kiutawala, yani kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)
na kuingia upinzani, pia sio sahihi kushinda kwa kurushiana mabomu na risasi za
moto.
Wapo
watu wanaocheka kwa vitendo hivi. Hao wanajidanganya kuwa muda wa mabadiliko
umefika. Sawa, lakini mabadiliko hayo yana manufaa gani kama watu wanapoteza
maisha?
Kwanini
tusifuate sheria na taratibu za kiungwana? Angalia, wabunge wa Chadema baada ya
kususia Bunge, walivamia jiji la Arusha, wakijifanya wao ndio wenye uchungu
kuliko wengine.
Hizi
ni janja za kisiasa tu. Hakuna jipya linaloweza kufanywa kwa amani kama watu
wanapita kwenye migongo ya wananchi, bila huruma na kuangamiza roho za ndugu
zetu na wengine kupata majeraha na kuharibu nguvu kazi ya Taifa.
Wapo
radhi watu wafe lakini wao waendelee kujulikana katika mitaa na kaya zetu. Wapo
radhi wafanye fujo wakiamini kuwa vyombo vya habari vitawaandika pamoja na
kupata mijadala kwenye mitandao ya kijamii, ambayo imejaza wanasiasa
uchwara.
Ni
wale wanaoacha mambo ya maana na kujadili upupu wa mabwana wakubwa hawa ambao
wengi wao wanaishi maisha yenye kila raha, wakati wanaowahadaa na kufariki
wanalala njaa, wanakufa masikini.
Wanadanganya
kila wawezalo. Wanafanya kila hira, lakini siku akitoka hapo anaingia tena
bungeni kwa ajili ya kutunisha mfuko wake kwa posho za serikali.
Kulikuwa
na haja gani ya viongozi wa Chadema kufanya mkutano bila kupewa kibali? Hizi si
janja za kutaka waandikwe? Mwisho wa siku wabunge watatu, akiwamo Tundu Lissu,
Joyce Nkya, Mustafa Akoonay wakikamatwa huku mwenyekiti wao, kinara wa yote
hayo, Mbowe akifanikiwa kutoroka.
Ametorokea
kusipojulikana. Watu wanajua ametoroka, walioandika wanaandika katika media zao.
Kesho akikamatwa au kujisalimisha polisi aandikwe tena.
Huku
ni kusumbua umma. Huku ni kutumia ujanja kujinufaisha kisiasa kwa mambo ya
kijinga kabisa. Watanzania tuyaseme haya ili kuelimishana kwa ajili ya Tanzania
yetu.
Taifa
linakabiliwa na changamoto nyingi mno. Bajeti ya mwaka 2013/2014 imetangazwa
huku ikishindwa kujibu namna gani wananchi wanaweza kuishi maisha
bora.
Kodi
kubwa itakuwa migongoni mwao. Bei za bidhaa zinazotumiwa na walalahoi
zimeongezwa mara dufu. Biadhaa kama vile mafuta ya dizeli, petrol zitawafanywa
wananchi waishi mashakani.
Kuongezwa
kwa kodi hizo, kutaongezeka mfumko wa bei mara dufu. Nauli zitapanda na vyakula
havitakatika. Watu watakufa njaa. Hapa ndipo tunapohitaji vichwa vya wabunge
wetu, badala ya kuelemea kwenye mambo ya anasa, kupiga soga na kulinda umaarufu
wao usipotee.
Tunayasema
haya hata tutaitwa makada wa CCM au wale wanaombiwa wapo kwenye ndoa, yani
wananchi wanaounga mkono siasa za Chama Cha Wananchi (CUF).
Nadhani
kwa kulijua hili tunapaswa kuwa makini zaidi. Tuambiane ukweli, maana
kinachoendelea leo jijini Arusha, kitakuwapo tena katika mikoa yetu, wilaya au
vijiji vyetu.
Kama
leo wanaokufa ni Wachaga wanaounga mkono Chadema, basi kesho sumu hiyo itahamia wilayani
Handeni, Korogwe, Lushoto, maana nao wanafuatilia masakata haya yanayofanywa kwa
makusudi kama njia ya kulisumbua Taifa letu.
Nachukizwa
na vitendo vya kihuni. Natamani sheria ichukuwe mkondo wake. Kwa wale wanaofanya
uhuni wa aina hii wakibainika wakamatwe na kufunguliwa mashtaka au kuvifuta
vyama vya aina hii.
Najua
hili ni jambo litakalozusha ghasia na machafuko, maana watakimbilia kwenye
huruma za wananchi, lakini akheri ya pengo kuliko jino bovu.
Chadema
ni kero na lazima wajirekebishe, maana wanachofanya sasa, akipatikana kiongozi
makini, asiyekuwa na woga na anayesimamia vyema sheria zake, wanasiasa wengi
kwenye vyama vya aina hii wanastahili kutulizwa mihemko yao.
Mungu
ibariki Tanzania.
+255
712053949
+255
753806087
Mwisho
Post a Comment