PAMOJA na
kutowekwa wazi sababu rasmi ya kuachwa kwa kipa Juma Kaseja, imebainika kwamba
ni kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao Yanga.
Simba
ilipokea kipigo hicho, katika mchezo wa funga dimba wa Ligi Kuu Bara uliopigwa
Mei 18 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Kaseja Ndiye aliyekaa
langoni.
Sports Lady Blog imezinyaka habari za
kuaminika toka ndani ya uongozi wa Simba zinaeleza kwamba, kitendo kile kimewaudhi
sana viongozi kwani mabao aliyofungwa yalionbekana dhahiri kuwa yalitokana na
uzembe wake.
Kiongozi
mmoja wa Simba aliliambia gazeti hili kwamba, pamoja na mapungufu yote
aliyonayo Kaseja lakini walikerwa zaidi
na kufungwa kwake.
“Hivi
unavyomfahamu wewe Kaseja anaseweza kufungwa mabao kama yale, kwa kweli hilo
limetacha na maswali mengi kichwani, imetkera sana mwache aende zake,”alisema
Akienda
mbali zaidi, kiongozi huyo ingekuwa vizuri zaidi kama Kaseja angeweza kuonesha
umahiri wake na kuondoa dhana mbovu dhidi yake, lakini kitendo cha kukubali
nyavu zake kutikiswa kilitoa jawabu juu ya maswali walitokuwa nayo.
Hivi
karibuni kumekuwa na utata juu ya Kaseja kusajiliwa tena kwenye kikosi cha
Simba baada ya mkataba wake kumalizika huku baadhi wakitaka aongezwe na wengine
wakipinga.
Hata hivyo,
Mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage, Kaimu Makamu Joseph Itang’are
‘Kinesi’ na Mwenyekiti wa kamati ya usajili, zakaria Hanspoppe kwa nyakati
tofauti walisema Kaseja hawezi kuongezwa mkataba.
Viongozi hao
walitoa kauli hizo bila ya kueleza wazi sababu za kumuacha kipa huyo namba moja
wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambaye ameitumikia klabu hiyo karibu miaka 10.
Huku hayo
yakiendelea, Kaseja mwenyewe ameendeklea kukaa kimya na hata alipotafutwa kuzungumzia
hilo hakuwa tayari.
Na Dina Ismail wa Sports Lady blog
Post a Comment