Leo
asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la
kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa
kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka
wa serikali.CHANZO JFORAM.
Baada ya kufunguliwa shtaka
hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie
mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya
mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa
kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua
kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya
kujibu.
Muda huu ndio wanaondoka mahakamani, Sugu, Lissu na baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA ambao walikuwa mahakamani hapo
on Saturday, June 29, 2013
Post a Comment