HATIMAYE Mkoa wa
Mbeya umepata mwakilishi wa kushiriki kinyang’anyiro cha Mrimbwende wa Redds Miss Tanzania baada ya
shindano la kumpata Miss Mbeya
kukamilika.
Mratibu na Mwandaaji Miss Redds Mkoa wa Mbeya Gabriel Mbwile
amesem jumla ya warembo 12 wameshiriki kinynganyiro hicho tangia wawekewe kambi
hadi siku ya shindano.
Ameongea kuwa mshindi wa kwanza amezawadiwa kitita cha fedha
taslimu Milioni moja, mshindi wa pili
750,000/=, mshindi wa tatu 500,000/= na wengine wote wamepewa kifuta jasho cha shilingi 100,000/=.
Amewataja washindi hao kuwa ni Jackline Luvanda mshindi wa
kwanza, Aneth Brayton mshindi wa pili na Daina
Athlimani aliyeibuka msindi wa tatu.
Amewatja washiriki wengine kuwa ni Naba Magambo, Zainabu
Matabi, Salma Abdalah, Flaviana Sixbert, Sarah Samwel, Aisha Beneka, Darlin
Athani, Mwajabu Ngobai na Neema Raymond.
Aidha Mgeni rasmi katika kinyang’anyiro hicho Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani, amezidi kusisitiza suala la
amani kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwamba inapaswa kushughulikiwa ni kila mtu.
PICHA NA MBEYA YETU
Post a Comment