Msimamizi
wa mradi huo, akitoa maelezo kwa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013
ambao waliambatana na Madiwani wa Viti Maalum kutembelea ofisi ya wakala
wa Usafiri wa Haraka zilizoko Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Ziara
ya warembo hao ilikuwa na nia ya kuwajengea uwezo warembo hao waweze
kutambua miradi mbali mbali inayoendeshwa na serikali.
Warembo
wa Redd's Miss Kinondoni 2013 wakimsikiliza Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi
ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo mara baada ya
kutembelea ofisi kwake.
Kaimu
Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi.
Astelia Mrambo akitoa maelezo kwa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013
juu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa
mwaka 2014 ambapo mpaka sasa baadhi ya vituo na karakana zimeshaanza
kukamilika.
Kaimu
Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi.
Astelia Mrambo akiwa na mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni
2013 wakiwaongoza warembo kuangalia ujenzi wa vituo vya mabasi yaendayo
kwa haraka kituo hicho kilichokatika hatua za mwisho kukamilika kipo
Manzese jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi.
Astelia Mrambo akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya mradi huo.
Maelezo yakiendelea kutolewa...
Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akifanya mahojiano na vyombo ya habari.
Mshiriki wa Redd's Miss Kinondoni 2013 akieleza machache waliyojifunza.
CREDITS: SUFIANI MAFOTO BLOG
Post a Comment