Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NAIBU WAZIRI ATOA RAI KWA WASTAAFU WA NSSF


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kulia) na  Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe ya siku ya wanachama wastaafu (Pensioners) wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 Wastaafu.
 Wastaafu wakijiandikishankabla ya kuingia katika ukumbi wa Karimjee leo.
Baadhi ya wastaafu wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe ya siku ya wanachama wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Crescentius Magori. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa sherehe ya siku ya Wanachama wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga na Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume. 
Mstaafu wa NSSF, Justina Lyela akitoa ushuhuda wa athari za fao la kujitoa wakatti wa sherehe za wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Mstaafu akichangia wakati wa sherehe hizo.

Dar es Salaam, Tanzania

WASTAAFU nchini wametakiwa kuwa mabalozi wazuri kwa familia na jamii inayowazunguka, kuelewa faida na hasara ya Fao la Kujitoa, linalokimbiliwa na wanachama wa Mifuko ya Pensheni kwa Wastaafu, licha ya ukubwa wa athari zake.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Milton Mahanga, wakati wa sherehe ya Siku ya Wanachama Wastaafu (Pensioners) wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini.

Mahanga alisema kuwa, Fao la Kujitoa ni changamoto ni changamoto kubwa inayoikabili mifuko mingi ya pensheni nchini likiwamo NSSF na kwamba, jamii inapaswa kuepuka kukimbilia kujitoa pale wanapobadilisha ajira kutoka sehemu moja kwenda nyingine au ajira zao zinapokoma.

“Ni vema wastaafu au wanachama wanaohama au kubadili ajira zao wakaendelea na kuchangia hata wanapokuwa katika ajira binafsi, kuliko kukimbilia kujitoa ili kuchukua kilicho chao, ambacho umaliza muda mfupi baadaye na kuishi maisha ya kuhangaika,” alisema Mahanga.

Mahanga akawahikikishia wastaafu maisha bora baada ya kazi na kusema kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kumebeba dhima ya kufanikisha hilo, ambapo kazi zake ni kusimamia mifuko yote ya jamii nchini ili iweze kutoa huduma bora kwa wanachama wake.

“Hakuna anayeweza kubisha kuwa maendeleo tuliyonayo sasa nchini yametokana na kazi nzuri ya wastaafu katika sekta ya umma na binafsi na nguvu zao ndio zimelifikisha hapa taifa kimaendeleo, hivyo kuwathamini wastaafu ni kujali mchango wao, aliongeza Mahanga.

Aidha, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori aliwashukuru wastaafu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuhudhuria sherehe hizo, huku akiahidi hirika kuendelea na juhudi za kuwaelimisha waajiri ili kila mmoja ajue wajibu alionao kwa wanachama wake na haki zake katika NSSF.

Magori aliongeza kuwa, nia ya kuwa na siku kama hiyo ni kuonesha namna ushirikiano baina ya wastaafu na NSSF ulivyo na wigo mpana usio na mwisho, ambapo hafla za kukutana baina ya pande hizo hizo mara moja kwa mwaka huzaa awazo endelevu yenye tija kwa kila upande
 
IMECHOTWA: HABARI MSETO BLOG
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top