JESHI LA ULINZI LA WANANCHI
WA TANZANIA
03 Juni,
2013
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
limepata ujumbe kupitia simu za mkononi
ambao umesambazwa kwa wananchi mbalimbali ukisadikishwa kuwa unatolewa na JWTZ.
Ujumbe huo wa simu ya mkononi unasema ‘Habari
zilizotufikia hivi punde. Mtanzania yeyote, kaa makini usiokote kitu chochote
ambacho una shaka nacho, kunabomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi zaidi ya
30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la
chai chenye rangi ya fedha. Usiguse’
Piga namba
0756 000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo. Imetolewa na JWTZ’.
JWTZ
linapenda kuwaondoa wananchi hofu kutokana na taarifa hiyo. Kwanza, Ujumbe huo
haujatolewa na JWTZ. JWTZ haliwezi likatumia
mfumo huo wa SMS kuwapa wananchi wake taarifa za hatari kama hizo. Aidha, JWTZ
hutangaza kupitia vyombo rasmi kama vile Magazeti, Radio na Television.
Pili, bomu
la tani 100 ni zito mno, halijawahi kutengenezwa
duniani. Na kama lipo, haifahamiki bomu hilo litarushwa vipi , kwa kutumia
ndege au
Mzinga?. Lakini pia, mzinga wa aina hiyo haupo duniani
kote na wala hakuna ndege yenye uwezo huo, hasa kwa bomu lenye umbile dogo kama
hilo(Chupa ya Chai).
Tatu, habari
hizi hazina ukweli kisayansi wala kiuhalisia au fikra za kawaida. Tunawaomba
wananchi wazipuuzie taarifa hizi kwani sio za kweli ni uongo mtupu. JWTZ lipo
kwa ajili ya Wanachi hivyo, kwa taarifa hizi za hatari,lazima lingewajulisha
wananchi kwa njia zilizoelezwa hapo juu na si kwa simu za mkononi.
Imetolewa
na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Post a Comment