KIPA wa Simba, Juma Kaseja, amesema kwa sasa hawezi
kujiunga mapema katika mazoezi ya kikosi hicho kutokana na kwamba hana mkataba
na klabu yoyote.
Kauli hiyo ya Kaseja inakuja kufuatia kipa huyo mkongwe
kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba, ambao ulifikia tamati mwishoni mwa
msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Jumatano,
Kaseja alisema kwa sasa hawezi kujiunga mapema na kikosi hicho alichokitumikia
hadi msimu uliopita kwa kuwa hana mkataba na timu hiyo baada ya ule wa awali
kumalizika.
Kaseja
alisema kwa sasa atakuwa na mapumziko ya siku chache baada ya kumaliza majukumu
ya Taifa Stars, ambapo atajua hatima ya timu atakayoichezea msimu ujao ndani ya
siku saba kuanzia juzi.“Ukiniuliza
nitajiunga lini katika mazoezi ya Simba, sidhani kama nitakupa jibu zaidi ya
sijui, kutokana na sasa sina mkataba wowote na Simba, mimi sasa ni mchezaji
huru, mkataba wangu na Simba ulishakwisha,” alisema Kaseja huku akiongeza kwa
kusema:
“Hivi ninavyoongea na wewe (juzi jioni), ndiyo kwanza hata nyumbani
kwangu sijafika, natoka katika kambi ya timu ya taifa, nataka kwanza nikapumzike
kwa siku kadhaa na baada ya hapo nadhani ndani ya siku saba nitajua nini nifanye
na wapi nitasaini.”
Source.Champion.
on Thursday, June 20, 2013
Post a Comment