Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM), Abdulrahman Kinana
Na Nathan Mtega,Songea
VIONGOZI wa chama cha mapinduzi
wametakiwa kuacha kusimamia vitendo vya dhuluma ndani ya chama na nje ya chama
kwa sababu kufanya hivyo ni kukiua chama kama ilivyotekea katijka baadhi ya
maeneo nchini ikiwemo wilaya ya Songea mjini ambapo chama cha mapinduzi
kimepoteza kata nane katika chaguzi mbali mbali za
udiwani.
Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa
chama cha mapinduzi taifa Abdulraman Kinana wakati akizungumza na viongozi wa
chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa kwenye ufunguzi wa mkutano
wa wajumbe wa mkutano huo ambao ni pamoja na mabalozi wa nyumba kumi uliofanyika
kwenye uwanja wa Maji maji mjini Songea ambapo alisema kuwa vitendo vya dhuluma
ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya viongozi na watendaji dhidi ya
wanachama ndivyo vinavyokigharimu chama.
Alisema kuwa vitendo hivyo vya
dhuluma vimekuwa vikijitokeza zaidi nyakati za uchaguzi kwa kutumia lugha ya
kupanga safu kwa ajili ya manufaa ya kundi fulani bila kuzingatia matakwa ya
wanachama na hivyo wanachama huamua vinginevyo na kusababisha chama kushindwa
katika chaguzi ambazo vitendo hivyo viliendekezwa na mfano ni jimbo la Songea
mjini mkoani Ruvuma.
Aidha katika hatua nyingine Kinana
aliwataka watendaji wa chama kuacha tabia ya umangimeza kwa kutumia muda mwingi
kukaa ofisini na kutatua matatizo na kero za wananchi wakiwa ofisini bila kufika
kwenye maeneo ambayo wanachama na wananchi wapo na kero za muda mrefu
zinazohitaji utatuzi wao.
Alisema kuwa watendaji wanapaswa
kwenda mara kwa mara kwa wanachama kuwailikiliza maoni na mawazo yao badala ya
kukaa ofisini na kukutana na kundi dogo ambalo hutoa taarifa zisizo sahihi
kuhusu mwenendo wa chama kwenye baadhi ya maeneo aliongeza kuwa yeye ameamua
kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kuona na kufuatilia utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya chama cha mapinduzi na mkoani Ruvuma atarudi tena kwa ajili ya kazi
hiyo.
Naye Mbunge wa jimbo la Songea
mjini na Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi akifunga mkutano huo alisema
kuwa nchi ya Tanzania ni moja na inatakiwa iendelee kuwa moja bila kujali
iktikadi za kidini na kisiasa lakini kundi ambalo halitaki nchi iendelee kuwa
moja na serikali haitavumilia vitendo vya aina
hiyo.
Alisema kuwa utawala wa sheria
ndiyo unaopaswa kuungwa mkono na kila mmoja mwenye mapenzi mema na nchi kwa
sababu ndiyo msingi wa nchi ulioasisiwa na waasisi wa taifa na ndiyo
uatakaoendeleza utaifa na si vinginevyo,pia alimshukuru katibu mkuu Kinana kwa
kazi nzuri anayoifanya ya kurudisha na kuimarisha uhai wa chama
Post a Comment