Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini Timu ya Taifa (Taifa
Stars) akisalimiana na mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu
wakati wa hafla fupi ya kuzungumza na wachezaji jana kabla ya mechi
dhidi ya Ivory Coast. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki.
**********
Na Mwandishi wetu
Wadhamini
wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium Lager wamewaomba
watanzania washikane na kuungana pamoja wakati wa mechi dhidi ya Ivory
Coast kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwani kuna
watanzania ambao tayari wamekata tamaa.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (pichani)alisema
Taifa Stars inatakiwa kuungwa mkono na kushangiliwa kwa nguvu kwani
wachezaji wameonesha kuwa wana uwezo.
“Hawa
ni wanajeshi wetu…nawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi…tuwape
sapoti na tuoneshe uzalendo kwani kwenye mpira lolote linawezekana,”
alisema.
Bw
Kavishe alisema watanzania lazima welewa timu hii bado ni changa na ina
wachezaji wapya wenye umri mdogo ambao wameonesha uwezo mkubwa.
“Hata
ikitokea tusifuzu kwenda Kombe la Dunia, vijana wameshaonesha dalili
nzuri na tuna imani tutafanya vizuri katika mashindano mengine kama
AFCON na CHAN,” alisema.
Aliwataka
wachezaji kutulia uwanjani na kutobabaishwa na ukubwa wa timu ya Ivory
Coast kwani wana uwezo wa kuwafunga na kushangaza dunia nzima Jumapili.
“Hii
ni kama fainali kwa Ivory Coast na wao pia wamebabaika na kuitilia
maanani kabisa mechi hii kwa sababu tukiwafunga ina maana hawatakuwa na
uhakika wa kufuzu katika hatua inayofuata,” alisema Kavishe.
Bia
ya Kilimanjaro Premium Lager imetimiza mwaka mmoja tangu ianze
kuidhamini Taifa Stars na wadau mbalimbali wamesifia udhamini huu kwani
umeleta mabadiliko makubwa katika timu ya Taifa.
Timu
ya Ivory Coast iliwasili nchini Alhamisi usiku na imeweka kambi katika
hoteli ya Bahari Beach, Kunduchi tayari kwa mechi itakayopigwa katika
Uwanja wa Taifa JUmapili hii saa tisa kamili.
Kwa
mujibu wa TFF maandalizi yote yamekamilika na mechi hii inatarajiwa
kuangaliwa na maelfu ya watanzania watakaojitokeza uwanjani na kupitia
runinga pia.
Ivory
Coast inaongoza katika kundi C ikiwa na pointi 10, Tanzania ya tatu na
pointi 6, Morocco ya tatu na pointi 5 na Gambia ni ya nne na pointi 1.
Post a Comment