Katika habari zilizotawala uwanja wa
Tehama kwa wiki hizi ni habari ya Snowden, mfanyakazi wa shirika la
usalama la marekani (NSA) pia ni muajiriwa wa zamani wa CIA aliyelikisha
taarifa za siri zinazoelezea jinsi marekani inavyofuatilia taarifa za
watumia mtandao bila idhini yao. Kuna wanaomuona Snowden kama hero na
wengine wanamuona kama msaliti. Kulingana na maelezo ya Snowden kama alivyonukuliwa na mtandao wa Guarnian,
inamaana kila unachoongea, unachotuma kinachunguzwa, wanafanya hivi
kila mahali hadi kwa washika dau wakuu kwenye hii nyanja ambao ni
Facebook na Google. Taarifa inaelezea kuwa, mashirika haya yametakiwa
kuwapa NSA uwezo wa kuingia kwenye mitambo yao na kuchota
chochote wanachotaka bila taarifa ya ziada.
Siku chache zilizopita niliwahi kupata nafasi ya kuzungumza na professor mmoja anayejihusisha sana na mambo ya tafiti za mitandao hapa China, tulizungumza mengi, ila moja ya topiki ya mazungumzo ilikuwa ni kuhusu sababu za China kuzuia na kuendelea kuzuia mitandao mikubwa kama Google, Facebook, Twitter nk. Yeye alisema, sio tu kuwapa nafasi wataalamu wa nyumbani toka ushindani wa mataifa makubwa kama marekani bali pia hakuna kuaminiana kati ya nchi hizi mbili. Ukweli ni kuwa, kuna mambo mengi sana yanayoendelea nyuma ya panzia.
Aliongelea mambo mengi, pia akanigusia suala la vikwazo kwa Huawei, malalamiko ya marekani kufanyiwa uspy na China nk. Hivyo, kitu kimoja nilichojifunza hapa ni kuwa, jamaa wanajuana na ndio maana hawaaminiani. Nilipomuuliza je kuna sababu nyingine yoyote, alijibu, "Ken ding ya" akimaanisha haswaa. Sababu nyingine aliyoelezea ni kuwa ni jambo la hatari endapo nchi haitokuwa na umiliki wa taarifa muhimu za watu wake, hivyo kitendo cha kuruhusu makampuni ya kichina kuwa na vitu vya inawasaidia kuwa na jeuri na uwezo wa kulinda vitu vyao. Hii ilinifanya nikumbuke lile vuguvugu la mapinduzi ya nchi za warabu (haswaa Tunisia) lilihamasishwa sana ndani ya Facebook.
Wakati ninatafakari na kutafuta baadhi ya reference kwa ajili ya makala hii, nikasema niende Facebook (ingawa ninajua kuwa ninafuatiliwa, hehe) ili nipate baadhi ya taarifa, nikakutana na picha kwenye ukurasa wa Masanja Mkandamizaji juu ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na JKT, kwakuwa mimi ni mmoja wa wapenzi namba moja wa JKT, nikasema ni ngoja nikasome majina ya hawa vijana, nilipofika kule, nikakutana na ujumbe mzito " Bandwidth Limit Exceeded". Hii ikanipa mwanga zaidi wa kufikiria katika mtazamo mwingine.
MWANANCHI
Post a Comment