Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKINDA::MKIKATAA BAJETI BUNGE LINAVUNJWA

 

Spika wa Bunge Anne Makinda juzi usiku alifunga mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali, huku akiwaonya wabunge kwa kunukuu baadhi ya vifungu vya Kanuni za Kudumu za Bunge inayoashiria kuwa ikiwa hawatopitisha bajeti hiyo Rais atalivunja Bunge.
Akiahirisha kikao cha 53 cha Mkutano wa 11 wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma juzi usiku, Spika Makinda alitaja Kanuni ya 107 (1) na (2) ambayo hutumika kukidhi matakwa ya Ibara ya 90 (2)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohusu Rais kulivunja Bunge.
Kanuni hiyo ya 107.(1) inaeleza: “Mjadala kuhusu Hotuba ya Bajeti ya Serikali utakapomalizika, Spika atalihoji Bunge ili litoe uamuzi wake wa kupitisha au kutokupitisha Bajeti ya Serikali ili kukidhi matakwa ya Ibara ya 90(2) (b) ya Katiba.”
Akinukuu kifungu hicho cha Katiba, Makinda alisema: “Rais hawezi kulivunja Bunge, isipokuwa kama Bunge litakataa kupitisha bajeti.”
Mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2013/14 umejadiliwa kwa siku nne kuanzia Jumatatu wiki hii ambapo Makinda alisema kuwa wote walioomba kuchangia walifanya hivyo wamekwisha.
“Nafunga mjadala wa Bajeti ya Serikali Kuu leo, wote walioomba na waliokuwepo wamekwisha,” alisema Spika
Makinda.
Hata hivyo, wakichangia hotuba hiyo, wabunge wengi walionyesha kupinga bajeti hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwamo misamaha ya kodi, ongezeko la kodi katika mafuta ya petrol na kodi ya umiliki wa laini za simu (Simcard).
Wabunge pia walipinga bajeti hiyo wakitaka sekta ya madini ichangie zaidi Pato la Taifa, kupitia na kurekebisha mikataba ya madini.
Hali hiyo huenda inazua hofu kuwa huenda wabunge wengi wakaipinga kwa kuipigia kura ya hapana.
Kifungu cha 107(2) cha Kanuni za Kudumu za Bunge inaelekeza kuwa uamuzi wa Bunge kupitisha au kutokupitisha Bajeti ya Serikali utafanywa kwa kupiga kura ya wazi kwa kuita jina la mbunge mmojammoja.
Jana Makinda alitangaza Jumatatu ijayo ya Juni 24 kuwa ndiyo siku ambapo wabunge watapiga kura kwa kuitwa majina mmojammoja ili kupitisha Bajeti ya Serikali au la.
Hata hivyo, kurejea kwa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani wa Chadema ambao hawakuchangia mjadala huo wa Bajeti Kuu ya Serikali, hata kuwasilisha Bajeti Mbadala, kunaongeza hofu kuwa huenda wabunge wote wa kambi hiyo wakaipinga.


Wabunge
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu kauli hiyo ya Spika, baadhi ya Wabunge walikuwa na mtazamo tofauti huku baadhi wakisema Bunge halijawa na meno ya kuisimamia Serikali.
Mbunge wa Lindi, Salum Barwany (CUF) alisema: “Bunge halijawa na meno ya kuisimamia Serikali, kanuni iliyopo na aliyoitaja Spika Makinda inakinzana na uamuzi wa Bunge; inaonekana kuwa Bunge siyo sehemu ya kuisimamia Serikali.
Aliongeza kuwa hali hiyo ni athari ya Bunge kuwa sehemu ya Serikali na kwamba ingawa wabunge wa upinzani wanaweza kuikataa, lakini wale wa chama tawala CCM wanabanwa wakilazimishwa kuiunga mkono.
Kwa upande wake Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla (CCM) alisema: “Ingawa mimi sikuunga mkono bajeti katika mchango wangu, wabunge wa chama tawala CCM, tunalazimika kupiga kura ya ndiyo ili kuilinda dola inayoongozwa na chama chetu.
Alifafanua: “Huu ni utaratibu wa kawaida wa mabunge yanayofuata mfumo wa Westminster, wa uelekeo wa itikadi, mfano hapa tuna kambi ya rasmi moja ya upinzani na Serikali. Upinzani una haki ya kukataa, lakini wabunge wote wa CCM lazima walinde dola.”
Naye Mbunge Sylvester Mabumba alisema hatua hiyo ya Spika inawaandaa wabunge kupitisha bajeti hiyo, kwani kutokuipitisha ni sawa na kuizuia Serikali isitekeleze mipango yake kwa mwaka ujao, hivyo Katiba inaruhusu Rais kulivunja Bunge.
Hata hivyo, jana katika kile ninachoweza kutafsiriwa kama ni kuwapiga mkwara wabunge wakati akiahirisha kikao cha Bunge, Spika Anne Makinda alitaka wabunge wote kuwapo bungeni Jumatatu ijayo kwa ajili ya kupiga kura akisema hata walio safarini ni lazima warejee na kushiriki upigaji kura huo muhimu.

MWANANCHI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top