Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MLIPUAJI BOMU ATAMBULIKA ARUSHA.

 


Mtoto ambaye alijeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu Arusha.
 
ARUSHA: 
MASHUHUDA wa tukio la mlipuko wa bomu uliotokea mwishoni mwa wiki iliyopita Jijini Arusha, wamedai kumwona na kumtambua mtu aliyehusika na tukio hilo lakini wanasema walishidwa kumkamata kutokana na “kushambuliwa kwa risasi na polisi”.
Mlipuko huo ulitokea katika Viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani jijini humo na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi zaidi ya 100.
Mashuhuda hao ambao wote walijeruhiwa kwa risasi wanasema mlipuaji wa bomu alikuwa amevalia shat
i la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans yenye rangi ya blue na kwamba wajihi wake ni mtu wa kimo cha kati.
Mmoja wa mashuhuda hao ni mlinzi katika Kikosi cha Ulinzi cha Chadema (Red Brigade) ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alidai kwamba alimwona mtu aliyerusha bomu mara tu baada ya tukio hilo.
Mlinzi huyo ambaye alipigwa risasi za mguuni na kifuani wakati akimkimbiza mtu huyo, alisema bomu hilo lililipuka mara tu baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia na kushuka jukwaani.
“Baada ya Mwenyekiti Freeman Mbowe kushuka jukwaani, nikawapanga walinzi kwa ajili ya kuwalinda viongozi waliokuwa wakichangisha fedha. Ghafla nikasikia mlipuko, sikujua ni nini, lakini kuna mama mmoja alikuwa karibu yangu akanionyesha mtu aliyelipua, akisema yuleee…” alisema na kuongeza.
“Alikuwa amevaa shati la kijivu lenye mistari myeusi na suruali ya jeans ya blue. Ni mtu wa kimo cha kati. Watu walianza kumkimbiza kuelekea upande wa Magharibi wa Uwanja kwenye nyumba za NHC. Tuliruka uzio alipopita yule mtu, mara nikasikia risasi imenipata mguuni.”
“Tulikuwa na uwezo wa kumkakata yule mtu, lakini nikaona risasi zimezidi upande wetu nikaona nigeuze na hapo hapo nikapigwa risasi ya kifuani, nikaishiwa nguvu, sikuweza kufahamu mtu huyo alikoishia. Nilijikongoja na kurudi uwanjani.”
Mlinzi huyo ambaye amelazwa katika moja ya hospitali za jijini Arusha anasema alilazimika kuhama hospitali ya Seliani alikokuwa amelazwa awali baada ya kuandamwa na polisi. “Nilikaa siku tatu hospitalini bila kupata huduma yoyote, lakini kila siku madaktari walikuwa wakinihoji maswali,”alisema na kuongeza.
“Mwisho nikaambiwa kwamba nitahamishiwa ghorofa ya chini, nilipouliza sababu wakasema eti Waziri Mkuu atakuja kuniona… Niligoma mwisho daktari akaniambia kuwa kuna polisi waliovaa majoho ya udaktari ndiyo waliotaka nihamishwe”.
Maelezo yake yanafanana na yaliyotolewa na majeruhi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Alila ambaye alisema kuwa alimwona mtu aliyelipua bomu “akiingia kwenye gari la polisi”.
“Baada ya mlipuko, sikujua kama nimeshapigwa risasi, lakini niliona watu wakimkimbiza mtu baada ya mama mmoja kusema kuwa ndiye aliyerusha bomu. CHANZO MWANANCHI.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top