Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu akiwaonyesha
waandishi wa habari miwani yake aliyodai kuvunjiwa na polisi. Lissu alipata
dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati, jijini Arusha jana baada ya
kukamatwa juzi. Picha na Moses Mashalla.
ARUSHA/DAR ES
SALAAM.
WABUNGE wanne wa Chadema, ambao waliachiwa na polisi kwa dhamana wamesimulia mateso waliyoyapata wakiwa rumande baada ya kukamatwa juzi.
WABUNGE wanne wa Chadema, ambao waliachiwa na polisi kwa dhamana wamesimulia mateso waliyoyapata wakiwa rumande baada ya kukamatwa juzi.
Vigogo hao; Mbunge wa Mpanda Mjini Said
Amour Arfi, Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce
Mukya (Viti maalumu), walikamatwa juzi baada ya wao na wafuasi wa chama hicho
kutawanywa kwa mabomu
ya machozi na polisi kwenye Viwanja vya Soweto, Arusha.
Wabunge hao waliachiwa baada ya kujidhamini
wenyewe huku watu wengine 65 waliokamatwa pamoja nao wakiachiwa baada ya
kudhaminiwa.
Wote wanatakiwa kuripoti kwenye kituo hicho
Julai 22, mwaka huu na wataelezwa hatma ya suala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jeshi lake
linaendelea kuwasaka Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa
Arusha, Godbless Lema na kuwaonya kuwa wanatakiwa kujisalimisha mara
moja.
Chagonja alisema Mbowe na Lema wanatafutwa
kwa kosa la kufanya kusanyiko lisilo halali katika viwanja hivyo vya Soweto
walipokuwa wakitaka kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma
na Amir Ally waliofariki dunia baada ya kuumizwa kutokana na mlipuko wa bomu,
Jumamosi iliyopita.
Pia aliwaamuru Mbowe na Lema kuwasilisha
mara moja ushahidi wa kuwahusisha polisi na shambulio la bomu na kama hawana
imani na Polisi, basi wawasilishe ushahidi wao kwa Rais Jakaya
Kikwete.
Lissu
Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, alilalamikia kitendo cha polisi kumwagia maji ya
kuwasha baada ya kumkamata.
“Walinimwagia maji ya kuwasha kwa mfululizo
nikalazimika kulala chini kifudifudi huku nikiwa nimefunika macho kukwepa
yasiingie maji. “Kuna askari walitaka kunipiga lakini niliokolewa na mwenzao
mmoja aliyenikinga nisishambuliwe.
Kwa kweli ilikuwa hali ya hatari,” alisema.
Kwa kweli ilikuwa hali ya hatari,” alisema.
Alisema polisi hao waliomkamata walivunja
miwani yake kwa makusudi akisema aliikabidhi kaunta ikiwa
haijavunjika.
“Wakati naingia mahabusu nilikabidhi miwani
yangu lakini ajabu wakati tukiachiwa ilikuwa imevunjika.” Alilalamikia hatua ya
polisi kuwashambulia kwa mabomu, kuwamwagia maji ya kuwasha walipokuwa
wakiwatawanya watu waliokusanyika Soweto akisema awali, waliwaruhusu.
CHANZO
MWANANCHI.
Post a Comment