![]() |
| Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa kitandani hospitalini |
Akielezea kupigwa kwake,
Mbunge Joshua Nassari akizungumza na Mbowe na Nyalandu hospitalini hapo,
alisema alikuwa kwenye kata yake ya uchaguzi lakini ghafla alizingirwa na watu
zaidi ya 30.
Alisema katika kundi pia walikuwamo watu watatu wenye asili ya Kisomali ambao wawili kati yao ni wakazi wa jimbo lake la Arumeru.
“Walinishambulia na kunipiga hali iliyonilazimu kukimbilia kwenye gari langu na kutoa bastola ili kujihami, lakini wakati nakimbia nilizidiwa nguvu na watu hao na kuamua kukimbia sehemu asiyoijua ili kuokoa uhai wangu,” aliongeza Mbunge huyo.



Post a Comment