John Mnyika (MP) |
Na
Mwanablog
Pamoja na
kuwa wana ushahidi wa Picha, Mikanda ya Video inayoonyesha jinsi Polisi
walivyoshiriki kulipua bomu la Arusha, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
wamesema hawapo tayari kupokea pesa zilizotengwa na serikali kwa ajili ya mtu
atakayetoa taarifa kuhusu waliohusika na mlipuko wa
Arusha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Ofisi za Chama hicho Makao Makuu, Msemaji wa Chama hicho
John Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo alisema “hata kama bado hatujakaa
kama Chama kuafikiana suala hili, hizo pesa kuzichukua ni ufisadi tu, matumizi
mabaya ya pesa, serikali imepata wapi pesa za kulipa milioni mia kwa watoa
taarifa wakati haijawahi hata kutoa rambirambi kwa mjane wa Daudi Mwangosi,
licha ya kwamba Polisi walihusika kwa asilimia zote katika kuua, hatuwezi
kuhuchukua hizo pesa.
Kwanza
ifahamike kwamba serikali imeamua kutenga hilo fungu ili kuhalalisha matumi
mabovu ili kuhalalisha ulaji wa pesa, ije iseme tuliwalipa watoa taarifa, huu ni
uongo, na serikali inapokuwa inadanganya raia wake inakosa uadilifu wa kuendelea
kutawala.
Suala la
Arusha ni tete, serikali imekuwa ikisema uongo hapa na pale, ndio maana hata
Mizengo Pinda tangu aseme uongo suala hilo halijawahi kuzungumzwa Bungeni, Spika
analipiga danadana kila mara.
Aidha
katika mkutano huo, Mnyika amelitaka jeshi la polisi liwaachie vijana watatu
wanaoteswa na Jeshi hilo ili kuwalazimisha kutoa mikanda waliyorekodi ambayo
Mbowe anasema wanayo inayoonyesha jinsi Polisi walivyolipua bomu, kuwapiga
risasi watu waliotaka kumkamata aliyelipua bomu, na gari ya polisi iliyomtorosha
mtu aliyerusha bomu. Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia vijana watatu
makada wa Chadema, ili liweze kupata mikanda hiyo kwa nguvu bila kutumia njia za
kuwaomba.
Post a Comment