HALI
ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema) Joshua Nassari,aliyehamishiwa
juzi katika Hospitali ya Taifa ya Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)
jijini Dar es Salaam, akitokea Hospitali ya Silian jijini Arusha,
inaendelea kuimarika.
Mbunge
huyo alipigwa na watu aliowaita kuwa ni wanachama wa CCM Juni 16 mwaka
huu kwenye vurugu za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Makuyuni Wilayani
Monduli Mkoani Arusha.
Akizungumza na mtandao huu kwa
njia ya simu, msemaji wa MOI Almas Jumaa, alisema kuwa hali ya Mbunge
huyo, kwa sasa inaendelea kuimarika ingawa bado analalamika kuwa anahisi
maumivu makali shingoni na mgongoni, lakini bado anaendelea kuwa chini
ya uangalizi wa madaktari.
“Hali
ya mgonjwa inaendelea kuimarika ingawa bado analalamika maumivu ni
makali eneo la shingoni na mgongoni,kuna vipimo ambavyo amefanyiwa na
madaktari wake wanaendelea kuvitafiti ili kubaini tatizo zaidi,”alisema
Jumaa.
Akizungumzia
hali yake, Nassari alisema amepimwa kipimo cha X-ray ambapo kimeonyesha
kuwa pingili za mgongo wake zipo sawa, lakini daktari ameshauri
afanyiwe kipimo kingine kiitwacho MRI ili kuangalia hali ya mishipa
kutokana na maumivu makali anayoendelea kuyapata.
CREDITS: MAFOTO BLOG
Post a Comment